advanced Search

HAZINA YA MASWALI (MPANGILIO WA KIMAUDHUI:Tabia)

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

 • hebu tufafanulieni umuhimu wa Hadhithi Kisaa (Hadithi ya joho)
  3747 Elimu ya Hadithi 2012/05/23
  Hadhithi Kisaa (Hadithi ya joho) ambayo imenukuliwa ndani ya kitabu cha Sheikh Abbas Qummiy kijulikanacho kwa jina la Mafaatiihul-jinaan, ni Hadithi iliyobeba ndani yake ujumbe mzito wenye umuhimu wa aina mbili. Umuhimu wa kwanza ni kule Hadithi kuwa na fungamano la moja kwa moja na suala la uimamu na uongozi, ...
 • je hivi mnaweza mkanipatia baadhi ya Riwaya zenye kukataza kuwepo kwa mahusiano baina ya msichana na mvulana?
  3375 Sheria na hukumu 2012/06/17
  Msichana na mvulana wanaweza kuwa na aina mbali mbali za mahusiano ndani ya jamii ya wanaadamu, na bila shaka baadhi ya mahusiano hayo huwa si mahusiano salama na si halali. Kwa kweli swali lililo ulizwa na muulizaji wetu, ni swali lisilokuwa la wazi, lakini sisi tutalijibu swali hili kupitia aina ...
 • nini maana ya itikafu
  4489 Tabia kimtazamo 2012/05/23
  Neno (itikafu) kilugha, huwa lina maana ya kule mtu kukaa na kubaki katika sehemu au pahala maalumu, huku akiwa ameshikamana na jambo maalumu ndani ya mahala hapo, lakini neno hili kitaalamu (kwenye fani ya sheria za Kiislam) linamaanisha kule mtu kukaa katika sehemu takatifu kwa ajili ya kutaka kujikaribisha kwa ...
 • kwa nini tuwe wakalidi (wafuasi)?
  1844 Sheria na hukumu 2012/05/23
  Ruhusa ya kumfuata ulamaa maalumu katika matendo ya ibada za kila siku, inatakiwa kutolewa na akili ya mtu mwenyewe. Na wala ruhusa hiyo haingojewi kutoka kwa Maulamaa, huku kila mmoja akielewa umuhimu wa suala hili ndani ya maisha yake ya kila siku. Katika hali yakawaida, mtu huwa ana sababu mbili zinanomfanya ...
 • ni nani aliyeuzika mwili mtukuffu wa Imamu Husein (a.s)?
  2362 تاريخ بزرگان 2012/05/23
  Mitazamo ya maulamaa ni yenye kutofautiana kuhusiana na suala hili. Moja kati ya mitazamo hiyo, ni ule mtazamo unaowafikiana na baadhi ya Riwaya pamoja na vitabu vya Tarehe, mtazamo huu ni kama ifuatavyo: mwili wa Imamu Husein (a.s), umezikwa na mwanawe mpenzi na muaminifu, naye ni Imamu Zeinul-Aabidiin (a.s), ambaye ...
 • ni kwa nini maombolezo ya Imamu Husein (a.s), yakapewa jina la Raudha?
  2768 تاريخ کلام 2012/05/23
  Neno (Raudha) ni neno maalumu linalotumiwa na waombolezaji wa mwauwaji ya Imamu Husein (a.s), na neno hili linatoka kwenye kitabu maarufu cha maombolezo ya Imamu Husein (a.s), kijulikanacho kwa jina la (Raudhatush-Shuhadaa), na kitabu hichi ni moja kati ya vitabu vya mwanzo vilivyonukuu tokeo la Karbala, na mwandishi wa kitabu ...
 • hivi mvuta sigara aweza kuvuta sigara hali akiwa amefunga?
  1783 Sheria na hukumu 2012/05/23
  Wanazuoni wote wa Kifiqhi wanasema kuwa: ni wajibu wa kila mwenye funga kuchukuwa tahadhari, na kutofikisha kitu chochote kile kama vile tumbaku au moshi wa sigara ndani ya koo yake.[1] Na hakuna hata mmoja miongoni mwa wanazuoni aliyetoa ruhusa ya kuvuta sigara ndani ya funga, kwa hiyo basi ni lazima mtu ...
 • nini hukumu ya kupiga sindano ya nguvu au kutia maji ya nguvu (Intravenous injection) mwilini ndani ya Ramadhani?
  2288 Sheria na hukumu 2012/05/23
  Wanazuoni wamekhitalifiana kuhusiana na suala hilo. Kwa kupata jawabu tosha, ni lazima utuambie kuwa wewe ni mfuasi wa mwanazuoni gani? Ili tuweze kukupa jawabu makini zaidi. Kwa vyovyote vile mitazamo ya baadhi ya wanazuoni wetu ni kama iuatavyo: Bahjat (r.a) na Khameneiy (Mungu amuhifadhi), wanasema: iwapo sindano hizo zitakuwa ni kwa ...
 • ni zipi funga zilizo zisizofaa kwa mtazamo wa imam Shafi, Hanafi na Maalik?
  3350 Sheria na hukumu 2012/05/23
  Masiku yasiyofaa kufunga saumu mbele ya imam Abu Hanifa ni: siku ya idi ndogo na idi kubwa, pia kufunga siku ya mwezi 11, 12 na 13 ya mwezi wa Dhil-hijja, pia kufunga ndani ya idi pili hadi nne za idi ya mfunguo tatu. Funga zisizofaa kwa mtazamo wa imam Shafi ni: ...
 • tafadhalini tupeni ufafanuzi kuhusu mapokezi na maandiko ya Ziara ya siku ya Ashura.
  2617 Elimu ya Hadithi 2012/05/23
  Rejeo mama na asili hasa zinazo aminika ambazo zimeyanukuu maandiko ya Sala na salamu (Ziara) za siku ya Ashura ni vitabu viwili, navyo ni: kitabu Kaamiluz-ziaaraat cha Jaa'far bin Muhammad bin Quulewaihi Qummiy, ambaye amefariki mwaka 348 Hijiria, na cha pili ni kitabu kiitwacho Misbaahul-mujtahid cha Sheikh Tusiy aliyezaliwa ...

YALIYOSOMWA ZAIDI

MAFUNGAMANO