KAGUA
876
Tarehe ya kuingizwa:2012/05/10
Summary Maswali
ni namna gani Qur-ani imelielezea fungamno juu ya imani na kupatikana kwa utulivvu wa moyo?
SWALI
ni vipi Qur-ani imelielezea fungamano la imani na utulivu wa moyo unaoweza kupatikana kupitia fungamano hilo? Naomba pia muiashirie Aya na Sura yenye kuzungumzia fungamano hilo.
MUKHTASARI WA JAWABU

Kilugha panapotumika neno Imani au itikadi, humaanisha kule mtu kukubali na kusadiki, na maana hii huwa ni kinyume cha neno kukadhibisha na kukanusha. Kitaalamu neno imani huwa linamaanisha kule mtu kusadiki na kuamini jambo fulani kimatamshi, kimoyo pamoja na kimatendo, lakini neno utulivu ambalo ni tafsiri ya neno "اطمینان" lililoko kwenye lugha ya Kiarabu, huwa linamaanisha ile hali kupoa kwa moyo na kupata utulivu na kuepukana na fazaa zilizo ukumba moyo huyo kabla ya utuivu huo.

 

Tofauti baina ya imani na utulivu

Pale mtu fulani anapotatizwa na jambo fulani, yawezekana yeye akatumia dalili na njia za kimantiki ili ajithibitishie kuwa yeye yuko kwenye ukweli na usawa, na hilo linaweza kuiridhisha akili yake, lakini bado mara nyingi watu wenye kufanya jambo kama hilo, huonekana kuwa nyoyo zao bado ziko katika hali ya wasi wasi. Lakini iwapo moyo wa mtu utakuwa umeridhika na hali halisi ya matokeo au yale mambo yanayomtatiza, au kuridhika na ufafanuzi wake alioutumia katika kulitatua jambo hilo, hapo basi moyo wake utapata utulivu, naye ataepukana na wahaka wa moyo.

Tanapoziangalia Riwaya mbali mbali, tutakutia kuwa: moja ya yale maswali aliyoulizwa Imamu Ridhaa (a.s), lilikuwa ni kuhusiana na suala hili ambalo sisi tumo katika njia ya kulitafiti na kulipatia jawabu, ndani ya moja miongoni mwa Riwaya hizo, Imamu aliulizwa swali lifuatalo: (Je hivi Nabi Ibrahim (a.s) alikuwa na shaka fulani moyoni mwake? Imamu Ridha (a.s) alijbu kwa kusema: hapana, bali Nabi Ibrahim (a.s) alimuombo Mola wake amzidishie yakini zaidi, ili iwe ni nyongeza juu ya ile yakini yake aliyonayo).

JAWABU KWA UFAFANUZI

Neno imani kilugha huwa lina maana ya kusadiki, ambako huwa ni kinyume cha neno kukanusha,[1] na kitaalamu neno hili huwa lina maana ya kukiri na kukubali kwa matamshi, pamoja na kuwa na fungamano la imani hiyo kimoyo, vile vile kutenda matendo yaendayo sawa na imani hiyo ilivyo.[2] Ama neno "اطمینان" ambalo kwa Kiswahili ni lenye maana ya utulivu, kilugha huwa linaaanisha kupoa na kupata utulivu wa moyo au utulivu wa roho, baada roho au moyo huo kukumbwa na wahaka.[3]

 

Tofauti baina ya imani na utulivu wa moyo

Kuna baadhi ya wakati sisi huwa tunajaribu kuzikinaisha na kuzikubalisha nyoyo zetu kutokana na mambo fulani yanayotukereketa, mabadilisho ambyo huwa tanayafanya kupitia dalili za liakili na kimantiki, ili kuzifikia yakini na imani fulani ambazo sisi tayari tumesha amua kuzikubali na kujifunga nazo, lakini pia wengi miongoni mwetu huwa bado mioyo yao na roho zao zina wahaka na hazijaridhika na dalili hizo za kiakili au kimantiki.

Lakini pale sisi tunapokuwa tumeridhika na mambo hayo kupitia nyoyo zetu na kukubaliana na mabo hayo kiroho na kiimani, hapo basi tayari nyoyo zetu tutazikuta kuwa ni zenye kupata raha na utulivu ndani yake. Hali ambayo huziweka mbali nyoyo zetu kutokana na wahaka pamoja na wasi wasi; kwa mfano: sisi sote tunaamini kuwa maiti hawezi kumdhuru mtu na wala hawezi kutendo jambo fulani kama vile kuinuka, kutembea na kadhalika, ama kwa kutokana na wasi wasi tuliokuwa nao moyoni mwetu, kila mmoja wetu huwa ni mwenye kumkhofu maiti, na khofu hiyo huzidi zaidi pale mtu huyo anapokuwa karibu na maiti huyo katika nyakati za usiku huku yeye akiwa peke yake. Lakini kwa upande wa wale watu ambao ni wenye kuwa na mazoea ya kukaa na maiti mara kwa mara, wao huwa hawawaogpi maiti.[4] Kwa kweli moyo wa mtu huwa hautulii hadi pale mtu anapopata yakini kutokana na kile yeye kinachombughudhi au kumtatanisha. Nabii Ibrahim (a.s) alikuwa na imani kamili juu ya ufufuo na kuhuika tena kwa wafu, naye hakuwa na shaka ya aina yoyote ile kuhusiana na hilo, na kule yeye kumtaka Mola wake amuoneshe namna ya vile anavyowahusha na kuwafufua maiti, kulikuwa na nia ya kuifikia yakini kamili ya moyo wake juu ya jambo hilo.

Na katika Riwaya fulani, Imamu Ridha (a.s), aliulizwa na mtu fulani kuhusiana na hilo, na swali hilo lilikuwa ni kama ifuatavyo: je Ibrahim (a.s) alikuwa na shaka moyoni mwake? Imamu Ridha (a.s) alijibu: hapana, bali Ibrahim (a.s) alikuwa na yakini kamili, lakini alichokitaka kwa Mola wake, ni kuitimiza yakini ya moyo wake.[5]

Kuna Riwaya zenye kuonesha ubatili wa moja kwa moja juu ya fikra za wale wenye kuona kuwa: kwa sababu Ibrahim (a.s) alikuwa na shaka kuhusiana na ufufuo kisha akamuomba Mola wake amuoneshe dalili zitakazo utuliza moyo wake, basi na mimi pia nina haki ya kumtaka Mola anioneshe dalili maalumu zitakazonituliza moyo wangu.

Moja kati ya zile Riwaya zenye kuukata moja kwa moja mzizi wa fikra hizi, ni Riwaya ifuatayo:

Siku moja kuna mtu aliye muandikia Imamu Musa Kaadhi (a.s) barua na kumwambia: mimi niko katika hali ya shaka kama vile Ibrahim alivyokuwa na shaka  kisha akamuomba Mola wake kwa kumwambia: Ewe Mola; hebu nioneshe vile wewe unavyowafufua viumbe wako! basi mimi pia nina hamu ya kupata dalili kama alivyopata Ibrahim (a.s) kutoka kwa Mola wake! Hapo Imamu (a.s) aliijibu barua ya mtu huyo kwa maneno yafuatayo: Ibrahim (a.s) alikuwa ni muumini, kisha akapenda imani yake izidi na ipee zaidi, lakini wewe ni mwenye shaka na wala bado huko katika imani, na kwa kweli mtu mwenye shaka huwa haipatikani kheri kutoka kwake.[6]

Kwa hiyo mtu anatakiwa aamini na kuikiri misingi ya itikadi na imani pamoja na kuwa na yakini kamili juu ya misingi hiyo, na inabidi mtu azifuate njia za dalili madhubuti zitakazoweza kumsaidia katika kulithibitisha jambo hilo ili yeye ajisafishe na aepukana na shaka juu ya misingi hiyo, na hilo ndilo litakalomuokoa yeye kutokana na vikwazo vya maswali mbali mbali, naye pia anaweza kuwafuata wanazuoni ili kujipatia misingi hiyo kwa kupitia misingi madhubuti ya hoja na dalili imara.

Kwa hali yoyote ile, iwapo mtu atatafakari kwa kiasi fulani na akazisoma Aya za Qurani zenye kuhusiana na misingi ya imani, yeye ataweza kujitosheleza ipaswavyo, na pia atafahamu vyema kwamba: njia madhubuti ya kuepukana na urukwaji wa roho na kutokuwa na utulivu, ni kule mja kuikweza imani yake na kujikita ndani ya imani hiyo kisawa sawa. Pale muumini anapotambua na kudiriki kwamba rehema ya Mola wake ni yenye kumlinda na kumpa himaya, yeye huwa tayari anajihisi kuwepo kwenye ngao ya rehema ya Mola wake, na hilo huwa linamfanya yeye kuepukana na matatizo ya kisaikolojia pamoja na kutokuwa na utulivu wa moyo. Mwenye Ezi Mungu anasema:

" " و لا تهنوا و لا تحزنوا و انتم الاعلون ان كنتم مؤمنین. Maana yake ni kwamba: Msinyong’onyee wala msihuzunike na nyinyi ndiwo mlioko juu iwapo kweli mtakuwa ni waumini. Na Mola katika Aya mbali mbali, amesema wazi wazi kwamba: Iwapo nyinyi wanaadamu mtakuwa pamoja na Mola wenu, basi Mola wenu atakumilikisheni nguvu zote za mbinguni na ardhini, na pia Mola wenu ni mjuzi wa matatizo yenu yote mliyo nayo, Naye ni Mjuzi wa utiifu wenu na imani zenu. Vipi basi mja awe katika himaya kama hii, kisha bado yeye awe na wahaka wa moyo? Bila shaka njia zote zenye kumsababishia mwanaadamu mashaka na wahaka wa moyo huwa ni zenye kukomeshwa kupitia imani imara yenye nia safi.

 


[1] Lisanul-Arab, cha Muhammad bin Mukrim Ibnu Mandhuur, juz/13, uk/21, chapa ya Daarus-Saadir, Beirut, chapa ya tatu ya mwaka 1414 Hijiria.

[2] Al-Kaafi cha Koleiniy, juz/2, uk/27, chpa ya Daarul-Kutubil-Islaamiyya, Tehran, chapa ya mwaka 1365 Shamsia. Hadithi kutoka kwa Imamu Saadiq (a.s) yenye kuzungumzia suala hili ni kama ifuatavyo:

(الْإِيمَانُ هُوَ الْإِقْرَارُ بِاللِّسَانِ وَ عَقْدٌ فِي الْقَلْبِ وَ عَمَلٌ بِالْأَرْكَانِ،)

Kwa ufafanuzi zaidi rejea swali la 1311 katika tovuti yetu lenye kicha cha habari kisemacho: (sharti za imani na Uislamu), codi na kiungo cha swali tovutini ni: (1343), pia angalia swali la 5382 tovutini humo kicha cha habari kisemacho: (tofauti ya imani na elimu), kodi na kiungo cha swali katika tovuti hii ni: (5651).

[3] Mufradaatu Alfaadhil-Qur-ani, cha Husein bin Muhammad Raaghi Isfahaniy, kilichotarjumiwa na kuhakikiwa na Ghulam Ridha Khosrawiy, chapa ya Murtadhawiy, Tehran, chapa ya pili ya mwaka 1375 Shamsia.

[4] Tafsiri Nemune ya Nasir Mkarim Shirazi, juz/1, uk/330, chapa ya kwanza ya kitengo cha uchapishaji cha Taarikhul-Arabiy, Beirut, mwaka 1412 Hijiria.

[5] Nuruth-Thaqalaini, cha Abdu Ali bin Jum-a’ Aruusiy Huwaiziy, juz/1, uk/330, chapa ya kwanza ya taasisis  ya Taariikhul-Arabiy, Beirut, mwaka 1412 Hijiria.

[6] Rejea kitabu kilichopita, juz/1, uk/336.

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
Tafadhali ingiza thamani

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI

  • kuna tofauti gani baina ya tabia na eimu ya tabia (saikolojia)?
    1260 Tabia kimtazamo 2012/06/17
    Neno (tabia) linatokana na neno la Kiarabu (اخلاق) ambalo ni umoja wa neno (خُلْق) lenye maana ya tabia, nyenendo au sifa za watu mbali mbali zinazo zimbatana na matendo yao bila ya kutofautisha baina ya sifa na tabia mbaya na zile sifa njema. Wataalamu wa elimu ya tabia (saikolojia) na wanafalsafa ...
  • je ni kweli kuwa Maimamu ni wabora zaidi kuliko hata Mitume?
    1259 Elimu ya zamani ya Akida 2012/05/23
    Suala la Maimamu (a.s) kuwazidi Mitume katika daraja za kielimu, ni suala moja linalo onekana kuzungumziwa sana na Riwaya mbali mbali, na sababu hasa za wao kuwazidi Mitume kielimu, zinatokana na ule uhakika wa nuru ya maumbile yao, kwani uhakika wa nuru yao unatokana na uhakika wa nuru ya Mtume ...
  • kwa nini Imamu Husein (a.s) anaitwa Tharu-Llahi (ثار الله)?
    1232 Tabia kimtazamo 2012/05/23
    Neno Tharu-Llahi (ثار الله) limekuja likiwa na maana mbili: moja ni kwa maana ya damu, na ya pili ni kwa maana ya kulipiza kisasi na kutaka kummwga damu ya muuwaji. Kwa hiyo maana ya mwanzo inapotumika kwa ajili ya kumuita Yeye (a.s) Tharu-Llahi (ثار الله), huleta maana ya kuwa: Mola weke ...
  • nini maana ya neno (dini)? Au dini hasa ni kitu gani?
    1146 Falsafa ya Dini 2012/05/23
    Wamagharibi wametumia ibara mbali mbali ili kupata maana muwafaka inayowafikiana na neno (dini), na neno (dini) ndani ya Qur-ani limetumika huku likibeba maana mbili tofauti, nazo ni kama ifuatavyo: 1- dini ni aina yeyote ile ya itikadi yenye kulenga nguvu maalumu za ghaibu zinazoaminiwa na kundi fulani la waumini wa nguvu ...
  • kwanza kabisa napenda kuuliza kuwa: je watu wa Peponi wote watakuwa ni vijana? Na la pili ni kwamba: imekuwaje miongoni mwa Maimamu wote pamoja na Mtume (s.a.w.w), ikawa Imamu Hasan na Husein tu ndio mabwana wa vijana wa Peponi?
    1109 Elimu ya zamani ya Akida 2012/05/23
    Wajukuu hawa wawili wa Mtume (s.a.w.w) ni mabwana wenye utukufu juu ya vijana wote Peponi, haidhuru kuwa ndani ya Pepo watu wote watakuwa katika hali moja ya ujana, ama wao (Imamu Hasan na Husein (a.s)) ndio watakaong’ara zaidi katika wale vijana waliouwawa katika njia ya Mola, au wale waliofariki katika ...
  • kwa mtazamao wa Kiislamu, mwanaadamu ni kiumbe gani?
    1109 Elimu mpya ya Akida 2012/05/26
    Kwa mtazamo wa Qur-ani, mwanaadamu ni kiumbe aliyebeba sifa mbili tofauti za kimaumbile, moja ni ile inayotokana na maumbile aliyopewa tokea mwanzo kutoka kwa Mola wake, nayo ni maumbile ya kiroho, na ya pili inatokana na maumbile ya kiwiliwili alichonacho. Maumbile asili ya kiroho (kifitra), huwa ni yenye kiu ya ...
  • nini maana ya itikafu
    1107 Tabia kimtazamo 2012/05/23
    Neno (itikafu) kilugha, huwa lina maana ya kule mtu kukaa na kubaki katika sehemu au pahala maalumu, huku akiwa ameshikamana na jambo maalumu ndani ya mahala hapo, lakini neno hili kitaalamu (kwenye fani ya sheria za Kiislam) linamaanisha kule mtu kukaa katika sehemu takatifu kwa ajili ya kutaka kujikaribisha kwa ...
  • nini maana ya usemi usemao kuwa: kumzuru Imamu Husein (a.s) ni sawa na kumzuru Mola kwenye Arshi yake”?
    1082 Elimu ya zamani ya Akida 2012/05/23
    Imamu Husein bin Ali (a.s) ambaye ni Imamu wa tatu wa Kishia, ni mtu mwenye fadhila kubwa mbele ya Mola wake, na fadhila hizo amezipata kwa kutokana na malengo yake, matendo, kutojitanguliza mbele katika maslahi ya jamii yake pamoja na kule kujitoa keake muhanga kwa ajili ya dini na manufaa ...
  • nini maana ya ucha Mungu?
    1079 Tabia kimtazamo 2012/05/23
    Taqwa (ucha Mungu) ni nguvu maalumu za kiroho zinazo weza kupatikana ndani ya nafsi ya mwanaadamu, nguvu ambazo huwa ni himaya maalumu inayomuwezesha yeye kujitenga na maasi. Taqwa kamili ni ile inayomfanya mtu kujiepusha na maasi yanayo eleweka na kila mmoja wetu, pamoja na kujiepusha na yale yote yanayo dhaniwa ...
  • hivi ni kwa nini Imamu Ali (a.s), hakuamua kilinda nafsi yake mbele ya adui yake (Ibnu Muljim), hali ya kuwa Yeye (a.s) alikuwa akielewa vyema nia ya adui huyo?
    1043 Elimu ya zamani ya Akida 2012/05/23
    Jawabu kamili ya swali hili yaweza kukamilika kuvitambua vipengele vifuatavyo: Vigezo halisi kwa mja katika utendaji wa amali na nyadhifa zake zinazomfungamanisha na wanajamii mbali mbali, ni ile elimu yake ya kawaida. Imamu (a.s) huwa hatumii nguvu zake za ndani zinazotokana na utukufu wa roho yake ambazo ni zenye kushikamana na ulimwengu ...

MAFUNGAMANO