advanced Search
KAGUA
4593
Tarehe ya kuingizwa: 2012/04/10
Summary Maswali
katika nuio la ndoa ya muda mfupi, iwapo mwanamme atakuwa ni naibu na wakili wa mwanamke naye akalisoma nuio la ndoa baina yake na huyo mwanamke bila ya kutaja na kuainisha kiwango cha mahari na muda wa ndoa hiyo, je katika hali hiyo ndoa hiyo itakuwa imesihi?
SWALI
mimi nimeingia katika ndoa ya muda mfupi na mwanamme fulani, na mimi nilimuwakilisha yeye awe ni naibu wangu katika kuinuia ndoa hiyo, naye akaisoma na kuinuia ndoa hiyo bila ya kuainisha muda maalumu wala kiwango cha mahari ya ndoa hiyo. Je ndoa hii ni sahihi?
MUKHTASARI WA JAWABU

Jawabu kutoka kwa baadhi ya wanazuoni wetu ni kama ifuatavyo:

Ofisi ya kielimu ya Ayatu-Llahi Khamenei (Mungu amhifadhi) yenye kuhusika na kujibu maswali ya kifiqi, imetoa jawabu ifuatayo:

Iwapo mwanamke alimuakilisha mwanamme huyo kuisoma na kuinuia ndoa, pamoja na kumpa yeye uwakili wa kuainisha mahari pamoja na muda wa ndoa hiyo, ndoa hiyo haitakuwa na matatizo, lakini tu kinachotakiwa kuzingatiwa ni kwamba: ni wajibu kuchukua tahadhari katika kuifunga ndoa hiyo, yaani kunatakiwa zizingatiwe sharti za ndoa, na miongoni mwa sharti hizo, ni kutaka ruhusa kutoka kwa walii wa mwanamke, iwapo mwanamke huyo atakuwa ni bikra.

Ofisi ya kielimu ya Ayatu-Llahi Sistani (Mungu amhifadhi) yenye kuhusika na kujibu maswali ya kifiqi, imetoa jawabu ifuatayo:

Ndoa hiyo haina matatizo na imesihi.

Ofisi ya kielimu ya Ayatu-Llahi Makaarim Shirazi (Mungu amhifadhi) yenye kuhusika na kujibu maswali ya kifiqi, imetoa jawabu ifuatayo:

Iwapo mwanamme huyo alipewa unaibu wa kuifunga ndoa pamoja na unaibu wa kuainisha muda na mahari, basi ndoa yao itakuwa imesihi na haina mashaka.

Ofisi ya kielimu ya Ayatu-Llahi Safi Gulpegani (Mungu amhifadhi) yenye kuhusika na kujibu maswali ya kifiqi, imetoa jawabu hii:

Iwapo mwanamme atakuwa ameifunga ndoa hiyo kwa nia ya muda maalumu na mahari maalumu, lakini mwanamke akawa hana habari juu ya hilo, kisha mwamke huyo akapata habari baada ya muda fulani kuhusu kiwango cha mahari pamoja na muda halisi wa ndoa hiyo, ndoa yao itasihi.

Ofisi ya kielimu ya Ayatu-Llahi Mahdi Hadawiy Tehraniy (Mungu amhifadhi) yenye kuhusika na kujibu maswali ya kifiqi, imetoa jawabu ifuatayo:

Iwapo wewe (mwanamke) ulimpa huyo mwanamme uwakili wa yote hayo, yaani kuifunga ndoa pamoja na kuainisha muda na mahari, yaani wewe ulimpa mwanamme ruhusa ya kuanisha yeye mwenyewe muda anautaka na mahari anayo yataka. Ndoa yenu itakuwa ni sahihi, lakini iwapo wewe utakuwa hukumpa yeye aina hiyo ya uwakili na unaibu, basi usahihi wa ndoa hiyo utategemea ridhaa yako wewe baada ya wewe kujua na kufahamu kiwango cha mahari na muda wa ndoa alichokianisha mwanamme huyo, kwa hiyo kuridhika na kukubali kwako wewe juu ya hilo, ndiko kutakoifanya ndoa hiyo ipasi na iwe salama.

 

JAWABU KWA UFAFANUZI

Kwa ajili ya kunufaika zaidi kuhusiana na masuala ya ndoa ya muda mfupi, angalia maswali yafuatayo katika tuvuti yetu:

1- Swali namba 1238: kuhusiana na masharti ya ndoa za muda mfupi, namba ya swali kwenye tovuti ni 1225.

2- Swali namba 2190: kuhusiana na ndoa ya muda mfupi kwa aliyekuwa bikra, namba ya swali katika tovuti ni 2315.

2- Swali namba 3237: kuhusiana na ulipaji wa mahari ya ndoa ya muda mfupi, namba ya swali katika tovuti ni 3494.

4- Swali namba 7454: kuhusiana na kuyaelewa mashati ya ndoa ya muda mfupi, namba ya swali katika tovuti ni 7664.

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
Tafadhali ingiza thamani

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

 • nini hukumu ya funga kwa mjumbe anaye safiri kwa ajili ya kuufikisha ujumbe wa Alla (S.W) au kwa ajili ya kufanya kazi fulani?
  2722 شغل مسافرتی 2012/05/23
  watu kama hawa wanatakiwa kusali safari, na pia hawaruhusiwi kufunga katika hali kama hiyo, na wala hawawezi kufunga funga zao za nadhiri huku wakiwemo ndani ya mwezi wa Ramadhani tena safarini. Lakini iwapo wao wataifikia sehemu walioikusudia kwenda kubaki hapo kabla ya kukengeuka kwa jua, ...
 • je ni kweli kuwa Imamu Hsein (a.s) alifunga ndoa na bibi Shahre-Baanu?
  3532 تاريخ بزرگان 2012/05/23
  Suala la ndoa ya Imamu Husein (a.s) na bibi Shahre Baanu aliyetekwa na jeshi la Kiisalamu, ni suala liliozungumziwa na vitabu vya historia huku likiwa na rangi mbali mbali za Ibara zenye kutofautiana, baadhi ya kauli zimesema kuwa: yeye alitekwa katika zama za utawala wa Omar, huku ...
 • maadili mema yana nafasi gani kwenye uwanja wa mazoezi?
  4342 Tabia kimatendo 2012/05/23
  Uisalmu ni dini kamili iliyokusanya ndani yake mfumo kamili na salama wenye kutoa muelekeo wa kiutendaji kuhusiana na kipengele kimoja kimoja miongoni mwa vile vipengele vinavyo husiana na maisha ya mwanaadamu. Uislamu haukuliweka nyuma suala la afya ya mwili wa kila mmoja wetu. Kwa hiyo Uislamu ni ...
 • je ni kweli kuwa Malaika wameumbwa kupitia nuru ya Maimamu (a.s)? Na je ni kweli kuwa wadhifa wao ni kumlilia na kuomboleza mauwaji ya Imamu Husein (a.s)?
  4632 Elimu ya zamani ya Akida 2012/05/23
  1- Suala la Malaika kuumbwa kutokana na nuru ya watu fulani, ni suala maarufu lilinukuliwa kutoka kwenye Riwaya za pande zote mbili, za Masunni na Mashia. Ndani ya vitabu vya Kishia, kuna Riwaya zinazoelezea kuwa: Malaika wameumba kutokana na nuru za watu maalumu, kama vile: Mtume na ...
 • je kitabu cha tarehe kijulikanacho kwa jina la Taarekhu-Tabari, ni kitabu kinachoaminika?
  3363 تاريخ بزرگان 2012/05/23
  Pale kitabu fulani kinaposemekana kuwa ni chenye kuaminika, huwa haimaanishi kuwa kila kilichomo ndani yake ni sahihi. Kitabu Taarikhut-Tabariy, si chenye kuepukana na usemi huu, bali nacho pia hakikubeba ndani yake yale yalio sahihi tu. La pili ni kwamba: kauli hiyo ulioinukuu kutoka katika kitabu hicho ...
 • je Imamu Huein (a.s) aliwahi kuwa na bint aliyeitwa Ruqayya?
  2851 تاريخ بزرگان 2012/05/23
  Katika tokeo muhimu la Karbala, kulikuwa kuna aina nyingi za nyuso zilizong’ara, na baadhi ya nyuso hizo zilikuwa ni nyuso za watoto wadogo, lakini Tarehe haikunukuu habari kamili kuhusiana na nyuso zote za watoto hao. Lakini mmoja miongononi mwa watoto waliotajwa na Tarehe, ni Ruqayya mwana wa ...
 • Apakah para imam maksum (a.s) bermutʽah (perkahwinan sementara)?
  1905 Nyenendo za Waliotakaswa (a.s) 2014/04/20
  Perkahwinan sementara merupakan salah satu daripada sunnah-sunnah Islam yang telah diumumkan di dalam al-Qur’an[i] dan orang beriman boleh memanfaatkan perkahwinan ini sekiranya memerlukan dan menghendakinya. Sunnah yang baik ini terjadi di zaman Rasullah (s.a.w), khalifah pertama dan sebahagian dari zaman pemerintahan khalifah kedua sehinggalah ...
 • hebu tufafanulieni umuhimu wa Hadhithi Kisaa (Hadithi ya joho)
  4944 Elimu ya Hadithi 2012/05/23
  Hadhithi Kisaa (Hadithi ya joho) ambayo imenukuliwa ndani ya kitabu cha Sheikh Abbas Qummiy kijulikanacho kwa jina la Mafaatiihul-jinaan, ni Hadithi iliyobeba ndani yake ujumbe mzito wenye umuhimu wa aina mbili. Umuhimu wa kwanza ni kule Hadithi kuwa na fungamano la moja kwa moja na suala la ...
 • nini hukumu ya kufuga njiwa ndani ya sheria za Kiislamu? Na nini msingi hasa wa hukumu hiyo?
  8448 Sheria na hukumu 2012/06/17
  Tukilitazama suala la kufunga njiwa kibinafsi, tutalikutia kuwa suala hili halina matatizo na ni halali. Lakini pale sisi tutapolimbatanisha suala hili na haki za majirani au wanajamii, hapo tunaweza kulipa picha ya uhalali au uharamu kwa jinsi hali za jamii mbali mbali zinavyolitazama suala hilo. Baadhi ya ...
 • Timsahın saxlanılması və digər ölkələrə satışına icazə varmı?
  1528 Sheria na hukumu 2014/05/22
  Təqlid olunan müctehidlərin cavabları bunlardır: Həzrət ayətullah Xamnei (Allah qorusun) Əti haram olan heyvanların saxlanılması və onun hətta, bu heyvanların ətlərinin yeyilməsini halal bilənlərə də satılması düzgün deyildir. Amma, aqillər nəzərində halal mənfəətə görə olsa məsələn, ətinin başqa ət yeyən heyvanlar üçün istifadəsi yaxud, dərisinin dəri sənətində ...

YALIYOSOMWA ZAIDI

MAFUNGAMANO