Please Wait
9618
Ofisi ya kielimu ya Ayatu-Llahi Khamenei (Mungu amhifadhi) yenye kuhusika na kujibu maswali ya kifiqi, imetoa jawabu hii:
Iwapo wewe utakuwa katika mashaka makubwa kwa kutokana na kuwa na aina hiyo ya ngozi, basi unaruhusiwa kufanya upresheni kwa ajili ya kuitibu ngozi yako.
Ofisi ya kielimu ya Ayatu-Llahi Makaarim Shirazi (Mungu amhifadhi) yenye kuhusika na kujibu maswali ya kifiqi, imetoa jawabu ifuatayo:
Iwapo jambo hilo halitapelekea kutendeka jambo la haramu ndani yake, au kusababisha madhara mengine makubwa zaidi kulikoa haya aliokuwa nayo, hapo hapakutakuwa na tatizo, lakini iwapo kufanya hivyo kutapelekea kupatikana jambo fulani la haramu, kama vile kuguswa mwili wake au kukashifiwa na madokta, basi katika hali kama hii yeye hatoruhusiwa kufanya hivyo mpaka pale ambapo yeye atakuwa amelazimika kufanya hivyo kwa njia moja au nyengine, hapo tena yeye atakuwa hana budi kufanya hivyo.
Namba maalumu ya kuelekea kwenye uwanja wa masali na majibu ya kifiqhi, ni 1994.