Jawabu kutoka ofisi ya elimu ya AyatuLlahi Khamenei (Mungu amhifadhi): Iwapo kumfunga huko mimba kutakuwa ni mateso kwa mnyama huyo, basi jambo hilo halitofaa kutendwa. Jawabu kutoka ofisi ya elimu ya AyatuLlahi Mahdi Hadawiy Tehraniy (Mungu amhifadhi), ni kama ifuatavyo: Iwapo ...
Imamu Khomeiniy (r.a), alitilia mkazo sana katika mazungumzo yake ya mara kwa mara ya kwamba: muhanga wa Imamu Husein (a.s), pamoja kuadhimisha siku ya muhanga huo kwa kuandaa vikao vya maombolezo kwa ajili ya kuikumbuka kwa ajili ya kupata somo juu ya tendo hilo la Imamu Husein ...
Ndani ya fatwa za wanazuoni, kuna mambo 9 ya msingi yenye kubatilisha saumu, nayo ni: 1- kula na kunywa, 2- kujamii, 3- kupiga ponyeto, 4- kumzulia uongo Mola na Mtume wake pamoja na maimamu (s.a.w.w), 5- kuingiza vumbi zito kooni, 6- kuzamisha kichwa majini, 7- kubaki na ...
Dini ni chombo maalumu kilichokuja kumkomboa mwanaadamu na kumuongoza katika njia ya mafanikio, hivyo basi ni jambo lisiloingia akilini kuwa chombo hichi kiwe ni chenye kulipa mgongo jambo muhimu linalohitajika ndani ya jamii mbali mbali, kama vile suala la usimamishaji wa serikali. Na kwa upande mwengine ni ...
Wanazuoni wamekhitalifiana kuhusiana na suala hilo. Kwa kupata jawabu tosha, ni lazima utuambie kuwa wewe ni mfuasi wa mwanazuoni gani? Ili tuweze kukupa jawabu makini zaidi. Kwa vyovyote vile mitazamo ya baadhi ya wanazuoni wetu ni kama iuatavyo: Bahjat (r.a) na Khameneiy (Mungu amuhifadhi), wanasema: ...
Kwanza tuwie radhi kawa kuchelewa kukujibu swali lako. Tuna tazizo wakati mwengine la kuchelewa kujibu maswali kwa haraka, hii ni kwa kutokana na kuzidiwa na maswali, au wafanya kazi wetu kuto kuwa na muda wa kutosha katika kujibu maswali mbali mbali. ...
Kwa kweli hakuna kitabu miongoni mwa vitabu maarufu vya Tarehe vyenye kutegemewa kilichozungumzia na kuthibitisha suala la hali halisi juu ya wazee wa Maalik Ashtar, bali tu kinachofahamika kuhusiana nao, ni kuwa wao ni watu wa makabila ya (Nukha’a) na (Mudh-haj) yalioko huko Yemen, lililothibitika ndani ya ...
Wajukuu hawa wawili wa Mtume (s.a.w.w) ni mabwana wenye utukufu juu ya vijana wote Peponi, haidhuru kuwa ndani ya Pepo watu wote watakuwa katika hali moja ya ujana, ama wao (Imamu Hasan na Husein (a.s)) ndio watakaong’ara zaidi katika wale vijana waliouwawa katika njia ya Mola, au ...
Pale kitabu fulani kinaposemekana kuwa ni chenye kuaminika, huwa haimaanishi kuwa kila kilichomo ndani yake ni sahihi. Kitabu Taarikhut-Tabariy, si chenye kuepukana na usemi huu, bali nacho pia hakikubeba ndani yake yale yalio sahihi tu. La pili ni kwamba: kauli hiyo ulioinukuu kutoka katika kitabu hicho ...
Wamagharibi wametumia ibara mbali mbali ili kupata maana muwafaka inayowafikiana na neno (dini), na neno (dini) ndani ya Qur-ani limetumika huku likibeba maana mbili tofauti, nazo ni kama ifuatavyo: 1- dini ni aina yeyote ile ya itikadi yenye kulenga nguvu maalumu za ghaibu zinazoaminiwa na ...
Neno (tabia) linatokana na neno la Kiarabu (اخلاق) ambalo ni umoja wa neno (خُلْق) lenye maana ya tabia, nyenendo au sifa za watu mbali mbali zinazo zimbatana na matendo yao bila ya kutofautisha baina ya sifa na tabia mbaya na zile sifa njema.
Tukilitazama suala la kufunga njiwa kibinafsi, tutalikutia kuwa suala hili halina matatizo na ni halali. Lakini pale sisi tutapolimbatanisha suala hili na haki za majirani au wanajamii, hapo tunaweza kulipa picha ya uhalali au uharamu kwa jinsi hali za jamii mbali mbali zinavyolitazama suala hilo. Baadhi ya ...
Mafunzo na fiqhi ya Kiislamu yaligawika sehemu mbili tokea ndani ya kipindi cha mwanzo cha tarehe ya Kiislamu baada tu ya kufariki Mtume (s.a.w.w), kipindi ambacho kilikuwa ni kipindi cha mzozo katika suala la nani ashike ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w), hapo kukazaliwa aina mbili za fiqhi: ...
iwapo mtu atawajibikiwa kufunga mwezi wa Ramadhani, naye kwa makusudi akabakia na janaba hadi adhana ya asubuhi, anaweza yeye akatayamamu katika nyakati za mwisho kabisa kabla ya kuadhiniwa adhana hiyo badala ya kuoga, kwa kuwa wakati wa kuoga haupo tena, kisha aendelee na funga yake, na funga ...
Kuritadi ni kitendo cha wazi kabisa cha kutoka katika dini, na mara nyigi tendo hilo hutumika kama ni nyenzo ya kuwadhoofisha wengine kiimani na kuwafanya waache dini yao, na hatimae kuwatoa na kuwaweka nje ya dini. Wanaohukumiwa hukumu ya kuritadi, ni wale wanaolidhihirisha tendo hilo kwa wengine, ...
Mtu anaweza kupatwa na janaba katika hali mbili: ima itakuwa ni kabla ya adhana ya asubuhi au baada ya adhana ya asubuhi, lakini janaba tunalolizungumzia hapo ni lile janaba la dharura, kama vile dharura ya kuota, siyo la kupiga ponyeto au kujamii. Kukoga janaba kabla ...
Taqwa (ucha Mungu) ni nguvu maalumu za kiroho zinazo weza kupatikana ndani ya nafsi ya mwanaadamu, nguvu ambazo huwa ni himaya maalumu inayomuwezesha yeye kujitenga na maasi. Taqwa kamili ni ile inayomfanya mtu kujiepusha na maasi yanayo eleweka na kila mmoja wetu, pamoja na kujiepusha na yale ...
Neno (itikafu) kilugha, huwa lina maana ya kule mtu kukaa na kubaki katika sehemu au pahala maalumu, huku akiwa ameshikamana na jambo maalumu ndani ya mahala hapo, lakini neno hili kitaalamu (kwenye fani ya sheria za Kiislam) linamaanisha kule mtu kukaa katika sehemu takatifu kwa ajili ya ...
Neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر), humaanisha utafutaji wa hila au njia katika kulifikia jambo fulani, na yawezekana mtu kutafuta hila na njia za kuyafikia mazuri au mabaya. Ujanja wa Mungu: kuna Aya tofauti ambazo zimeliegemeza na kulinasibisha neno (ujanja مکر) ...