Ofisi ya Ayatullahi Sistani (Mungu ameweke) inajibu kwa kusema: Iwapo wewe ulikuwa hujui kuwa saumu ni wajibu, basi lipa tu hizo funga za miaka minane, na hakuna haja ya kuzilipia fidia. Ofisi ya Ayatullahi Makaarim Shiraziy (Mungu amuweke) nayo inajibu ...
Wanazuoni wote wa Kifiqhi wanasema kuwa: ni wajibu wa kila mwenye funga kuchukuwa tahadhari, na kutofikisha kitu chochote kile kama vile tumbaku au moshi wa sigara ndani ya koo yake.[1] Na hakuna hata mmoja miongoni mwa wanazuoni aliyetoa ruhusa ya kuvuta sigara ...
Miongoni mwa amri kuu alizoamriswha mja na Mola wake baada ya ile amri ya kumpwekesha Mola wake, ni kwatii wazazi wawili. Kuhusiana na swali lililoulizwa hapo juu, pamoja na hali halisi iliyotajwa ndani ya swali hilo, mtu anapokuwa amekabiliwa na hali kama ...
Hijja kilugha; Ni kukisudia na kukiendea kitu au jambo fulani.[1] Neno hijja Kisheria na kitaalamu; Neno hijja kisheria ni lenye kuashiria aina maalumu ya ibada yenye kutendeka mahala maalumu, kwa mfumo na wakati maalumu. Ibada hii inatakiwa kutendeka katika nyumba maalumu ya Mwenye Ezi ...
Fani ya Fiqhi iliyo katika nyanja za juu (iliyobobea), huwa inampa mtu uwezo maalumu wa kuzivua na kuziopoa hukumu kuu za kisheria kutoka katika machimbuko yake, ambayo miongoni mwayo ni zile ibara za Qur-ani na Hadithi takatifu, na jambo hilo (kuwa na uwezo wa kuziopoa hukumu) ni ...
Iwapo sisi tutailelekea Qur-ani Tukufu, kisha tukaiuliza Qur-ani swali lifualato: je sisi tumeumbwa kwa ajili gani? Hapa tutaiona Qur-ani ikitujibu kwa kauli ifuatayo: " وَ ما خَلَقْتُ الْجِنَّ وَ الْإِنْسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ. " Maana yake ni kwamba: (Mimi (Mola) sikumuumba mwanaadamu wa jini, ila ...
Katika lugha ya Kiarabu, -ambayo ndiyo lugha ya sheria ya Kiislamu- neno (pendo) linatokana na neno "حب". Ambalo lina maana ya kule mtu kuwa na mapenzi na mtu, kitu au jambo fulani. Lakini neno pendo, mapenzi au neno jengine lenye maana kama hii, linapotumika na kunasibishwa ...
Neno (tabia) linatokana na neno la Kiarabu (اخلاق) ambalo ni umoja wa neno (خُلْق) lenye maana ya tabia, nyenendo au sifa za watu mbali mbali zinazo zimbatana na matendo yao bila ya kutofautisha baina ya sifa na tabia mbaya na zile sifa njema.
Uisalmu ni dini kamili iliyokusanya ndani yake mfumo kamili na salama wenye kutoa muelekeo wa kiutendaji kuhusiana na kipengele kimoja kimoja miongoni mwa vile vipengele vinavyo husiana na maisha ya mwanaadamu. Uislamu haukuliweka nyuma suala la afya ya mwili wa kila mmoja wetu. Kwa hiyo Uislamu ni ...
Suala la mtu kuwa na khofu huku akiwa na matarajio ya kheri, na kwa upande wa pili akawa na mapenzi ya Mola wake, huwa si suala la kushangaza, kwa mambo hayo mawili hayapingani katika kuwepo kwake, kwani kuwepo kwa hali mbili kama hizo huwa ni jambo la ...
Wamagharibi wametumia ibara mbali mbali ili kupata maana muwafaka inayowafikiana na neno (dini), na neno (dini) ndani ya Qur-ani limetumika huku likibeba maana mbili tofauti, nazo ni kama ifuatavyo: 1- dini ni aina yeyote ile ya itikadi yenye kulenga nguvu maalumu za ghaibu zinazoaminiwa na ...
Neno (tabia) linatokana na neno la Kiarabu (اخلاق) ambalo ni umoja wa neno (خُلْق) lenye maana ya tabia, nyenendo au sifa za watu mbali mbali zinazo zimbatana na matendo yao bila ya kutofautisha baina ya sifa na tabia mbaya na zile sifa njema.
Tukilitazama suala la kufunga njiwa kibinafsi, tutalikutia kuwa suala hili halina matatizo na ni halali. Lakini pale sisi tutapolimbatanisha suala hili na haki za majirani au wanajamii, hapo tunaweza kulipa picha ya uhalali au uharamu kwa jinsi hali za jamii mbali mbali zinavyolitazama suala hilo. Baadhi ya ...
Mafunzo na fiqhi ya Kiislamu yaligawika sehemu mbili tokea ndani ya kipindi cha mwanzo cha tarehe ya Kiislamu baada tu ya kufariki Mtume (s.a.w.w), kipindi ambacho kilikuwa ni kipindi cha mzozo katika suala la nani ashike ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w), hapo kukazaliwa aina mbili za fiqhi: ...
iwapo mtu atawajibikiwa kufunga mwezi wa Ramadhani, naye kwa makusudi akabakia na janaba hadi adhana ya asubuhi, anaweza yeye akatayamamu katika nyakati za mwisho kabisa kabla ya kuadhiniwa adhana hiyo badala ya kuoga, kwa kuwa wakati wa kuoga haupo tena, kisha aendelee na funga yake, na funga ...
Mtu anaweza kupatwa na janaba katika hali mbili: ima itakuwa ni kabla ya adhana ya asubuhi au baada ya adhana ya asubuhi, lakini janaba tunalolizungumzia hapo ni lile janaba la dharura, kama vile dharura ya kuota, siyo la kupiga ponyeto au kujamii. Kukoga janaba kabla ...
Kuritadi ni kitendo cha wazi kabisa cha kutoka katika dini, na mara nyigi tendo hilo hutumika kama ni nyenzo ya kuwadhoofisha wengine kiimani na kuwafanya waache dini yao, na hatimae kuwatoa na kuwaweka nje ya dini. Wanaohukumiwa hukumu ya kuritadi, ni wale wanaolidhihirisha tendo hilo kwa wengine, ...
Taqwa (ucha Mungu) ni nguvu maalumu za kiroho zinazo weza kupatikana ndani ya nafsi ya mwanaadamu, nguvu ambazo huwa ni himaya maalumu inayomuwezesha yeye kujitenga na maasi. Taqwa kamili ni ile inayomfanya mtu kujiepusha na maasi yanayo eleweka na kila mmoja wetu, pamoja na kujiepusha na yale ...
Neno (itikafu) kilugha, huwa lina maana ya kule mtu kukaa na kubaki katika sehemu au pahala maalumu, huku akiwa ameshikamana na jambo maalumu ndani ya mahala hapo, lakini neno hili kitaalamu (kwenye fani ya sheria za Kiislam) linamaanisha kule mtu kukaa katika sehemu takatifu kwa ajili ya ...
Neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر), humaanisha utafutaji wa hila au njia katika kulifikia jambo fulani, na yawezekana mtu kutafuta hila na njia za kuyafikia mazuri au mabaya. Ujanja wa Mungu: kuna Aya tofauti ambazo zimeliegemeza na kulinasibisha neno (ujanja مکر) ...