advanced Search
KAGUA
33047
Tarehe ya kuingizwa: 2012/04/07
Summary Maswali
kuna tofauti gani baina ya tabia na eimu ya tabia (saikolojia)?
SWALI
kuna tofauti baina ya tabia na elimu ya tabia (saikolojia)?
MUKHTASARI WA JAWABU

Neno (tabia) linatokana na neno la Kiarabu (اخلاق) ambalo ni umoja wa neno (خُلْق) lenye maana ya tabia, nyenendo au sifa za watu mbali mbali zinazo zimbatana na matendo yao bila ya kutofautisha baina ya sifa na tabia mbaya na zile sifa njema.

Wataalamu wa elimu ya tabia (saikolojia) na wanafalsafa wametoa aina mbali mbali za maana na ufafanuzi kuhusiana na maana halisi ya tabia. Lakini maana kuu inayoweza kufahamika kutoka katika ibara mbali mbali za wanazuoni wa Kiislamu ni kwamba: (tabia ni hali au sifa za nafsi ya mwanaadamu), hali na sifa ambazo huwa ndio sababu ya kupatikana kwa aina maalumu ya matendo kutoka kwa mwanaadamu huyo).

Na hiyo si maana pekee iliyotolewa na wanazuoni wa Kiislamu kuhusiana na maana ya tabia, bali pia kuna wanazuoni wengine waliyofafanua maana ya tabia kupitia ibara nyengine, na miongoni mwao ni marehemu Neiraqiy, yeye katika kitabu chake kiitwacho (Jaamius-Saadaat), amesema: (elimu ya tabia ni fani maalumu yenye kutafiti sifa (hali) hatari (mbaya) pamoja na zile sifa njema, pamoja na kuhakiki juu ya uwezekano wa mtu kuipamba nafsi yake kupitia sifa bora ziwezazo kumuokoa yeye kutokana na zile sifa mbaya zenye kuangamiza.)

 

Ama kuhusiana na tofauti baina ya elimu ya tabia (saikolojia) na tabia zenyewe (morals), ni kwamba: tofauti zaweza kupatika katika njia na mitazamo mbali mbali kuhusiana na vitu viwili hivi, kwa hiyo tabia haziwezi kuingiliana na fani yenye kutafiti tabia, na kila moja huwa inashika mashiko yake maalumu katika kuwepo kwake.

 

JAWABU KWA UFAFANUZI

Neno tabia kilugha

Neno tabia katika mtazamo wa kilugha, linatokana na neno la Kiarabu

( (خلْقlenye maana ya tabia, nyenendo, sifa na mazoea, bila ya kutafautisha mazoea na tabia hizo katika uzuri au ubaya wake.[1]

Neno tabia kitaalamu

Wataalamu wa fani ya tabia na nyenendo (saikolojia) wametoa maana mbali mbali kuhusiana na tabia, na zifuatazo ni baadhi ya maana hizi:

  • Baadhi ya wataalamu wamesema kuwa: tabia ni sifa na picha maalumu iliyojengeka nayo nafsi ya mwanaadamu, picha na sifa ambazo huwa ni chimbuko la kupatikana kwa matendo maalumu yaendayo sawa na picha hizo, pasi na yeye kuhitajia tafakuri maalumu kabla ya kutenda matendo hayo.
  • Wengine hulitumia neno tabia huku wakikusudia zile sifa tu zenye kumpa mwanaadamu thamani na kumfanya yeye aonekana na hali halisi ya utu na ubinaadamu, na kinyume cha neno (tabia) mbele ya wanazuoni hawa, ni neno (kuto kuwa na tabia) au kukosa tabia na malezi.[2]
  • Mara nyengine neno tabia hulenga maana ya taasisi yenye kushughulikia tabia na maisha ya wanaadamu kiujumla.

Maana mbali mbali kuhusiana na neno hili, ni zenye kuleta uzito katika kutafuta suluhu kamili ya maana ya neno hili, na si rahisi kuweza kuzikusanya maana hizo zote zilizotajwan hapo juu katika kifungu kiwezacho kuleta maana moja, lakini kwa upande mwengine sisi tunaweza kupana maana moja kuu kupitia maana mbali mbali zilizotolewa na wanazuoni wa Kiislamu kuhusiana na neno hili, na hilo ni jambo linalowezekana, kwani ingawaje kuna tofauti ndogo ndogo ndani ya ibara hizo zilizotolewa na wanazuoni hao, lakini bado kuna uhusiano na uwiyano ndani ya maana zilizomo kwenye ndani yake. Hapa basi kupitia ibara hizo, sisi tunaweza kuibuka na maana isemayo kuwa: (tabia ni sifa na hali zilizomo ndani ya nafsi ya mwanaadamu, hali ambazo huwa ndiyo chimbuko la kupatikana kwa aina maalumu za matendo kutoka kwa mwanaadamu huyo); yaani iwapo nafsi hiyo itakuwa na sifa njema, matendo ya mtu yatakuwa ni mema, na iwapo sifa hizo zitakuwa ni mbaya, basi matendo ya mtu mwenye nafsi hiyo yatakuwa ni mabaya vile vile. Ni vyema basi kuzigawa tabia katika mfungu mbali mbali, kama vile tabia njema, mbaya na potofu, na tabia au sifa hizi zinaweza kuwa ni sifa za mpito au ni sifa sugu zilizokomaa.

 

Elimu ya tabia (saikolojia)

Pia kuna maana nyingi zilizotajwa katika kuifafanua fani ya tabia.

Kumepita juhudi mbali mbali kutoka kwa wataalamu wa Kimagharibi pamoja na wanazuoni wa Kiislamu zilizokusudia kuleta maana halisi na makini ya elimu ya tabia (saikolojia), na baadhi ya maana zilizoweza kupatikana ndani ya juhudi hizo ni kama ifuatavyo:

  1. Elimu ya tabia (saikolojia), ni fani maalumu yanye kushughulikia na kutafiti hali ya uwezekano wa kujijenga na kujipamba na tabia njema.[3]
  2. Wengine wamesema kuwa: elimu ya tabia (saikolojia) ni fani yenye kutafiti namna ya hali halisi ya maisha yalivyo.[4]
  3. Wengine wameipa elimu hii maana ile ile ya kilugha ya neno ya tabia (اخلاق). Wao wamesema kuwa: elimu ya tabia (saikolojia), ni fani ya utambuzi na utafiti juu ya mazoea, adabu na tabia za watu zilivyo.[5]
  4. Marehemu Neiraqiy kwenye kitabu chake (Jaamius-Saa’daat) amesema: (elimu ya tabia (saikolojia) ni fani yenye kuhusiana na utafiti wa sifa na mazoea yenye uwezo wa kuangamiza na yale yenye uwezo wa kuokoa, pamoja na kutafiti namna ya kujenga mazoea na sifa njema ndani ya nafsi, mazoea na sifa ambazo zitakuwa ndiyo muokozi na mgombozi kutokana na hali ya hatari anayokabiliwa nayo mtu mwenye sifa hizo mbaya za kuangamiza.[6]

Kutokana utafiti mbali mbali juu ya maana halisi ya fani hii kupitia mitazamo ya wanazuoni mbali mbali wa Kiislamu, hapa tunaweza kusema kuwa: fani ya tabia (saikolojia) kwa mtazamo wa wanazuoni wa Kiislamu, ni fani maalumu yenye kutafiti sifa njema na mbaya, pamoja na kufafanua pia kutoa maana juu ya kila moja kati ya sifa hizo, huku ikitafiti njia za kuzichuma sifa njema zitakazo muokoa mwanaadamu, na vipi mwanaadamu ataweza kujisafisha na sifa mbaya zenye maangamizo.

Kwa hiyo basi, maudhuu hasa zinayotafitiwa ndani ya fani hii: ni sifa njema na namna ya kuzichuma na kujipamba nazo, na sifa mbaya na njia ya kutengana nazo, huku ikizingatiwa kuwa: sifa zinazoweza kutafitiwa ndani ya fani hii, ni zile tu zenye fungamano la moja kwa moja na uhuru wa mwanaadamu ndani ya chaguo la matendo yake ya hiari.

Lengo na makusudio ya fani hii, ni kumfikisha mwanaadamu kwenye kilele cha ukamilifu na furaha za maisha ya milele, pamoja na kumuweka kwenye daraja yake halisi iliyokusudiwa kufikiwa na malengo ya kuumbwa kwake. Pia tunapenda kuwakumbusha wasomaji wetu kuwa, fani hii ya (saikolojia), ni yenye fungamano mdhubuti na fani ya (falsafa) kiujumla.

 

 

Maana madhubuti ya fani hii ya tabia (saikolojia) na tabia zenyewe

Tabia ni ile hali ua sifa mbaya na nzuri, na elimu ya tabia (saikolojia): ni fani yenye mfumo maalumu wa kutafiti vyazo vya sifa hizo, huku ikitoa muamko na muelekeo kuhusiana na sifa zinazopaswa kushikwa na zile zinazopswa kujitenga nazo.

 

Mwisho wa makala.

 


[1] Qaamus Qur-an, cha Sayyid ali Akbar, juz/2, uk/293, chapa ya sita ya Daarul-Kutubil-Islaamiyya, Tehran, mwaka 1371 Shamsia. Majmaul-Bahraini, cha Fakhrud-Diin Taariihiy, juz/5, uk/156, chapa ya Kitaabfuruushiy Murtadhawiy, Tehran, chapa ya tatu ya mwaka 1375 Shamsia.

[2] Kwa ajili ya ufafanuzi zaidi, angalia tovuti ya (حوزه نت).

[3] Akhlaq Naasiriy, cha Khoje Nasiiru-Diin Tusiy, uk/14,chpa ya Kitaabfuruushiye Islaamiyye Biy Taa, Tehran.

[4] Ashenaye-Baa-Ulume Islaamiy, cha Murtadha Mutahhariy, juz/2, uk/190, chapa ya Sadraa, Tehran, mwaka 1368 Shamsia.

[5] Akhlaq, cha Badrud-Diin Kitaabiy, kitabu ambacho ni tarjama ya kitabu cha Mr. Jean-Pierre, uk/53, chapa ya Amuzesh Wa Parwaresh, mwaka 1373 Shamsia.

[6] Jaamius-Saa’daat, cha Muhammad Mahdiy Neiraqiy, juz/1, uk/34, chapa ya Najaf, Matbaa’tuz-Zahraa, mwaka 1368 Hijiria.

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

  • je ni wajibu wangu kulipa fidia ya funga zilizonipita kwa kutokana na uzembe wa wazazi wangu?
    8361 قضای روزه و کفارات 2012/05/23
    Ofisi ya Ayatullahi Sistani (Mungu ameweke) inajibu kwa kusema: Iwapo wewe ulikuwa hujui kuwa saumu ni wajibu, basi lipa tu hizo funga za miaka minane, na hakuna haja ya kuzilipia fidia. Ofisi ya Ayatullahi Makaarim Shiraziy (Mungu amuweke) nayo inajibu ...
  • hivi mvuta sigara aweza kuvuta sigara hali akiwa amefunga?
    8168 رساندن دود و غبار غلیظ به حلق 2012/05/23
    Wanazuoni wote wa Kifiqhi wanasema kuwa: ni wajibu wa kila mwenye funga kuchukuwa tahadhari, na kutofikisha kitu chochote kile kama vile tumbaku au moshi wa sigara ndani ya koo yake.[1] Na hakuna hata mmoja miongoni mwa wanazuoni aliyetoa ruhusa ya kuvuta sigara ...
  • iwapo amri za baba zitapingana na za mama, mwana atakuwa na anawajibu gani katika hali kama hiyo?
    13724 نیکی به پدر و مادر 2012/05/23
    Miongoni mwa amri kuu alizoamriswha mja na Mola wake baada ya ile amri ya kumpwekesha Mola wake, ni kwatii wazazi wawili. Kuhusiana na swali lililoulizwa hapo juu, pamoja na hali halisi iliyotajwa ndani ya swali hilo, mtu anapokuwa amekabiliwa na hali kama ...
  • Tafadhali naomba munieleweshe, nini maana ya hijja kilugha?
    7525 بیشتر بدانیم 2018/01/24
    Hijja kilugha; Ni kukisudia na kukiendea kitu au jambo fulani.[1] Neno hijja Kisheria na kitaalamu; Neno hijja kisheria ni lenye kuashiria aina maalumu ya ibada yenye kutendeka mahala maalumu, kwa mfumo na wakati maalumu. Ibada hii inatakiwa kutendeka katika nyumba maalumu ya Mwenye Ezi ...
  • je kuutangaza mwezi ni jukumu la wanazuoni wote kwa ujumla, au ni jukumu tu la kiongozi (mwanafiqhi / kadhi) mkuu wa dini nchini?
    10014 رؤیت هلال و یوم الشک 2012/05/23
    Fani ya Fiqhi iliyo katika nyanja za juu (iliyobobea), huwa inampa mtu uwezo maalumu wa kuzivua na kuziopoa hukumu kuu za kisheria kutoka katika machimbuko yake, ambayo miongoni mwayo ni zile ibara za Qur-ani na Hadithi takatifu, na jambo hilo (kuwa na uwezo wa kuziopoa hukumu) ni ...
  • maisha ya kiucha-Mungu ni maisha ya aina gani? Je misngi ya maisha hayo haipingani na misingi mikuu ya maisha yetu?
    13619 بندگی و تسبیح 2012/05/23
    Iwapo sisi tutailelekea Qur-ani Tukufu, kisha tukaiuliza Qur-ani swali lifualato: je sisi tumeumbwa kwa ajili gani? Hapa tutaiona Qur-ani ikitujibu kwa kauli ifuatayo: " وَ ما خَلَقْتُ الْجِنَّ وَ الْإِنْسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ. " Maana yake ni kwamba: (Mimi (Mola) sikumuumba mwanaadamu wa jini, ila ...
  • Vipi mtu anaweza kuwa kipenzi cha Mwenye Ezi Mungu?
    8441 Tabia kimatendo 2019/06/16
    Katika lugha ya Kiarabu, -ambayo ndiyo lugha ya sheria ya Kiislamu- neno (pendo) linatokana na neno "حب". Ambalo lina maana ya kule mtu kuwa na mapenzi na mtu, kitu au jambo fulani. Lakini neno pendo, mapenzi au neno jengine lenye maana kama hii, linapotumika na kunasibishwa ...
  • kuna tofauti gani baina ya tabia na eimu ya tabia (saikolojia)?
    33049 Tabia kimtazamo 2012/06/17
    Neno (tabia) linatokana na neno la Kiarabu (اخلاق) ambalo ni umoja wa neno (خُلْق) lenye maana ya tabia, nyenendo au sifa za watu mbali mbali zinazo zimbatana na matendo yao bila ya kutofautisha baina ya sifa na tabia mbaya na zile sifa njema.
  • maadili mema yana nafasi gani kwenye uwanja wa mazoezi?
    12666 Tabia kimatendo 2012/05/23
    Uisalmu ni dini kamili iliyokusanya ndani yake mfumo kamili na salama wenye kutoa muelekeo wa kiutendaji kuhusiana na kipengele kimoja kimoja miongoni mwa vile vipengele vinavyo husiana na maisha ya mwanaadamu. Uislamu haukuliweka nyuma suala la afya ya mwili wa kila mmoja wetu. Kwa hiyo Uislamu ni ...
  • je kuna haja ya kumkhofu Mola au tunatakiwa kuwa na mapenzi Naye?
    10393 محبت و دوستی 2012/05/23
    Suala la mtu kuwa na khofu huku akiwa na matarajio ya kheri, na kwa upande wa pili akawa na mapenzi ya Mola wake, huwa si suala la kushangaza, kwa mambo hayo mawili hayapingani katika kuwepo kwake, kwani kuwepo kwa hali mbili kama hizo huwa ni jambo la ...

YALIYOSOMWA ZAIDI