Kuna baadhi ya vitabu vya Tarehe vilivyoeleza kuwa: ingawaje Yazidu alikuwa ana kila aina ya starehe alizozitayarisha kwenye nyumba yake, wakiwemo aina mbali mbali za wanawake, lakini bado alikuwa hatosheki, na hakuwa akiyafumba macho yake pale anapowaona wanawake waliojistiri wakitembea mitaani au wakiwa katika kazi zao za ...
Ingawaje wengi miongoni mwa waandishi wa Historia hawakukinukuu kisa cha kuwepo kwa mtoto huyo wa kike wa Imamu Husein (a.s) mwenye umri wa kiasi cha miaka mitatu au mine, aliyejulikana kwa jina la Ruqayya au Fatimatu Sughra na baadhi ya wakati akijulikana kwa majina yasiokuwa hayo, lakini ...
Sisi swali lako tumelifanyia utafiti, na kulisaka katika maandiko mbali mbali yanayoelezea msiba wa Imamu Husein (a.s), vile vile tumeangalia ndani ya kitabu maarufu kijulikanachoa kwa jina la Luhuuf cha Sayyid Ibnu Taawuus, lakini juhudi zetu zimeishia ukingoni, nasi hatukuweza kupata ithibati yeyote ili kuhusiana na sentensi ...
Kuna Aya na Riwaya mbali mbali zenye kuonesha kuwa hali na sura halisi za maumbile ya baadhi ya watu ni zenye kutafautiana na lile umbile lao dhahiri wanalo onekana nalo katika ulimwengu huu wa dhahiri. Na mabadiliko hayo huwa yanatokana na yale matendo ya watu hao yalivyo. ...
Imamu Husein (a.s) pamoja na wafuasi wake pale walipokuwa Karbala, walikuwa wakisoma mashairi maalumu yenye ibara za kivita, kwa ajili ya kuwahamasisha wanavita, pia Abul-Fadhlil-Abbaas alionekana mara zote katika siku ya Ashura kusoma aina mbali mbali za ibara na mashairi ya kuvutia kwa ajili ya uhamasishaji, mashairi ...
Tukitoa jawabu ya kiujumla jamala kuhusiana na swali hilo lililoulizwa hapo juu, tunasema kuwa: si katika zama za zamani au za hivi sasa tu, bali katika zama zote hakujawahi kutokea mtu aliyeweza kuja na maneno yenye kufanana na Qur-ani kiufasaha na kibalagha, bali ufasaha unao onekana ndani ...
Ayatu-Llahi Mhdi Hadawiy Tehraniy (Mungu Amhifadhi), amelijibu swali hili kwa kusema: Bila shaka Maimamu (a.s) ni wenye mamlaka kamili ya kuitawala na kuzisarifu za waumini, lakini kufanya hivyo huwa kunahitajia idhini ya Mola Mtukufu, hivyo basi wao (a.s) huwa hawafanyi hivyo isipokuwa kuwe na maslahi maalumu juu ...
Jawabu kutoka kwa baadhi ya wanazuoni wetu ni kama ifuatavyo: Ofisi ya kielimu ya Ayatu-Llahi Khamenei (Mungu amhifadhi) yenye kuhusika na kujibu maswali ya kifiqi, imetoa jawabu ifuatayo: Iwapo mwanamke alimuakilisha mwanamme huyo kuisoma na kuinuia ndoa, pamoja na kumpa yeye uwakili wa ...
watu kama hawa wanatakiwa kusali safari, na pia hawaruhusiwi kufunga katika hali kama hiyo, na wala hawawezi kufunga funga zao za nadhiri huku wakiwemo ndani ya mwezi wa Ramadhani tena safarini. Lakini iwapo wao wataifikia sehemu walioikusudia kwenda kubaki hapo kabla ya kukengeuka kwa jua, ...
Wamagharibi wametumia ibara mbali mbali ili kupata maana muwafaka inayowafikiana na neno (dini), na neno (dini) ndani ya Qur-ani limetumika huku likibeba maana mbili tofauti, nazo ni kama ifuatavyo: 1- dini ni aina yeyote ile ya itikadi yenye kulenga nguvu maalumu za ghaibu zinazoaminiwa na ...
Neno (tabia) linatokana na neno la Kiarabu (اخلاق) ambalo ni umoja wa neno (خُلْق) lenye maana ya tabia, nyenendo au sifa za watu mbali mbali zinazo zimbatana na matendo yao bila ya kutofautisha baina ya sifa na tabia mbaya na zile sifa njema.
Tukilitazama suala la kufunga njiwa kibinafsi, tutalikutia kuwa suala hili halina matatizo na ni halali. Lakini pale sisi tutapolimbatanisha suala hili na haki za majirani au wanajamii, hapo tunaweza kulipa picha ya uhalali au uharamu kwa jinsi hali za jamii mbali mbali zinavyolitazama suala hilo. Baadhi ya ...
Mafunzo na fiqhi ya Kiislamu yaligawika sehemu mbili tokea ndani ya kipindi cha mwanzo cha tarehe ya Kiislamu baada tu ya kufariki Mtume (s.a.w.w), kipindi ambacho kilikuwa ni kipindi cha mzozo katika suala la nani ashike ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w), hapo kukazaliwa aina mbili za fiqhi: ...
iwapo mtu atawajibikiwa kufunga mwezi wa Ramadhani, naye kwa makusudi akabakia na janaba hadi adhana ya asubuhi, anaweza yeye akatayamamu katika nyakati za mwisho kabisa kabla ya kuadhiniwa adhana hiyo badala ya kuoga, kwa kuwa wakati wa kuoga haupo tena, kisha aendelee na funga yake, na funga ...
Kuritadi ni kitendo cha wazi kabisa cha kutoka katika dini, na mara nyigi tendo hilo hutumika kama ni nyenzo ya kuwadhoofisha wengine kiimani na kuwafanya waache dini yao, na hatimae kuwatoa na kuwaweka nje ya dini. Wanaohukumiwa hukumu ya kuritadi, ni wale wanaolidhihirisha tendo hilo kwa wengine, ...
Mtu anaweza kupatwa na janaba katika hali mbili: ima itakuwa ni kabla ya adhana ya asubuhi au baada ya adhana ya asubuhi, lakini janaba tunalolizungumzia hapo ni lile janaba la dharura, kama vile dharura ya kuota, siyo la kupiga ponyeto au kujamii. Kukoga janaba kabla ...
Taqwa (ucha Mungu) ni nguvu maalumu za kiroho zinazo weza kupatikana ndani ya nafsi ya mwanaadamu, nguvu ambazo huwa ni himaya maalumu inayomuwezesha yeye kujitenga na maasi. Taqwa kamili ni ile inayomfanya mtu kujiepusha na maasi yanayo eleweka na kila mmoja wetu, pamoja na kujiepusha na yale ...
Neno (itikafu) kilugha, huwa lina maana ya kule mtu kukaa na kubaki katika sehemu au pahala maalumu, huku akiwa ameshikamana na jambo maalumu ndani ya mahala hapo, lakini neno hili kitaalamu (kwenye fani ya sheria za Kiislam) linamaanisha kule mtu kukaa katika sehemu takatifu kwa ajili ya ...
Neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر), humaanisha utafutaji wa hila au njia katika kulifikia jambo fulani, na yawezekana mtu kutafuta hila na njia za kuyafikia mazuri au mabaya. Ujanja wa Mungu: kuna Aya tofauti ambazo zimeliegemeza na kulinasibisha neno (ujanja مکر) ...