Kilugha panapotumika neno Imani au itikadi, humaanisha kule mtu kukubali na kusadiki, na maana hii huwa ni kinyume cha neno kukadhibisha na kukanusha. Kitaalamu neno imani huwa linamaanisha kule mtu kusadiki na kuamini jambo fulani kimatamshi, kimoyo pamoja na kimatendo, lakini neno utulivu ambalo ni tafsiri ya ...
Kwanza tuwie radhi kawa kuchelewa kukujibu swali lako. Tuna tazizo wakati mwengine la kuchelewa kujibu maswali kwa haraka, hii ni kwa kutokana na kuzidiwa na maswali, au wafanya kazi wetu kuto kuwa na muda wa kutosha katika kujibu maswali mbali mbali. ...
Katika lugha ya Kiarabu, -ambayo ndiyo lugha ya sheria ya Kiislamu- neno (pendo) linatokana na neno "حب". Ambalo lina maana ya kule mtu kuwa na mapenzi na mtu, kitu au jambo fulani. Lakini neno pendo, mapenzi au neno jengine lenye maana kama hii, linapotumika na kunasibishwa ...
Kuna Aya na Riwaya mbali mbali zenye kuonesha kuwa hali na sura halisi za maumbile ya baadhi ya watu ni zenye kutafautiana na lile umbile lao dhahiri wanalo onekana nalo katika ulimwengu huu wa dhahiri. Na mabadiliko hayo huwa yanatokana na yale matendo ya watu hao yalivyo. ...
Tokeo hilo linaweza kutokea katika sura tatu, nasi tutazifafanua sura hizo na kuzijibu kwa mujibu mitazamo ya maulamaa isemavyo. Na jawabu zetu ni kama ifuatavyo: 1- iwapo mtu ataacha kufunga kwa kutokana na maradhi, kisha maradhi hayo yakaendelea hadi akafikiwa na Ramadhani ya mwaka wa ...
Kwa mtazamo wa Qur-ani, mwanaadamu ni kiumbe aliyebeba sifa mbili tofauti za kimaumbile, moja ni ile inayotokana na maumbile aliyopewa tokea mwanzo kutoka kwa Mola wake, nayo ni maumbile ya kiroho, na ya pili inatokana na maumbile ya kiwiliwili alichonacho. Maumbile asili ya kiroho (kifitra), huwa ni ...
Ndani ya ibara zilizomo kwenye maandiko ya Sala na salamu za siku ya Ashura zijulikanazo kwa jina la Ziaratu-Aa'shuuraa, kuna ibara ya kuwalaani Banu Umayya wote kwa ujumla akiwemo mwana wa Yazidu. Huku baadhi ya wanatarehe mbali mbali wakionekana kuwatakasa baadhi ya watu wa ukoo wa ...
watu kama hawa wanatakiwa kusali safari, na pia hawaruhusiwi kufunga katika hali kama hiyo, na wala hawawezi kufunga funga zao za nadhiri huku wakiwemo ndani ya mwezi wa Ramadhani tena safarini. Lakini iwapo wao wataifikia sehemu walioikusudia kwenda kubaki hapo kabla ya kukengeuka kwa jua, ...
Neno (Raudha) ni neno maalumu linalotumiwa na waombolezaji wa mwauwaji ya Imamu Husein (a.s), na neno hili linatoka kwenye kitabu maarufu cha maombolezo ya Imamu Husein (a.s), kijulikanacho kwa jina la (Raudhatush-Shuhadaa), na kitabu hichi ni moja kati ya vitabu vya mwanzo vilivyonukuu tokeo la Karbala, na ...
Suala la mtu kuwa na khofu huku akiwa na matarajio ya kheri, na kwa upande wa pili akawa na mapenzi ya Mola wake, huwa si suala la kushangaza, kwa mambo hayo mawili hayapingani katika kuwepo kwake, kwani kuwepo kwa hali mbili kama hizo huwa ni jambo la ...
Wamagharibi wametumia ibara mbali mbali ili kupata maana muwafaka inayowafikiana na neno (dini), na neno (dini) ndani ya Qur-ani limetumika huku likibeba maana mbili tofauti, nazo ni kama ifuatavyo: 1- dini ni aina yeyote ile ya itikadi yenye kulenga nguvu maalumu za ghaibu zinazoaminiwa na ...
Neno (tabia) linatokana na neno la Kiarabu (اخلاق) ambalo ni umoja wa neno (خُلْق) lenye maana ya tabia, nyenendo au sifa za watu mbali mbali zinazo zimbatana na matendo yao bila ya kutofautisha baina ya sifa na tabia mbaya na zile sifa njema.
Tukilitazama suala la kufunga njiwa kibinafsi, tutalikutia kuwa suala hili halina matatizo na ni halali. Lakini pale sisi tutapolimbatanisha suala hili na haki za majirani au wanajamii, hapo tunaweza kulipa picha ya uhalali au uharamu kwa jinsi hali za jamii mbali mbali zinavyolitazama suala hilo. Baadhi ya ...
Mafunzo na fiqhi ya Kiislamu yaligawika sehemu mbili tokea ndani ya kipindi cha mwanzo cha tarehe ya Kiislamu baada tu ya kufariki Mtume (s.a.w.w), kipindi ambacho kilikuwa ni kipindi cha mzozo katika suala la nani ashike ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w), hapo kukazaliwa aina mbili za fiqhi: ...
iwapo mtu atawajibikiwa kufunga mwezi wa Ramadhani, naye kwa makusudi akabakia na janaba hadi adhana ya asubuhi, anaweza yeye akatayamamu katika nyakati za mwisho kabisa kabla ya kuadhiniwa adhana hiyo badala ya kuoga, kwa kuwa wakati wa kuoga haupo tena, kisha aendelee na funga yake, na funga ...
Mtu anaweza kupatwa na janaba katika hali mbili: ima itakuwa ni kabla ya adhana ya asubuhi au baada ya adhana ya asubuhi, lakini janaba tunalolizungumzia hapo ni lile janaba la dharura, kama vile dharura ya kuota, siyo la kupiga ponyeto au kujamii. Kukoga janaba kabla ...
Kuritadi ni kitendo cha wazi kabisa cha kutoka katika dini, na mara nyigi tendo hilo hutumika kama ni nyenzo ya kuwadhoofisha wengine kiimani na kuwafanya waache dini yao, na hatimae kuwatoa na kuwaweka nje ya dini. Wanaohukumiwa hukumu ya kuritadi, ni wale wanaolidhihirisha tendo hilo kwa wengine, ...
Taqwa (ucha Mungu) ni nguvu maalumu za kiroho zinazo weza kupatikana ndani ya nafsi ya mwanaadamu, nguvu ambazo huwa ni himaya maalumu inayomuwezesha yeye kujitenga na maasi. Taqwa kamili ni ile inayomfanya mtu kujiepusha na maasi yanayo eleweka na kila mmoja wetu, pamoja na kujiepusha na yale ...
Neno (itikafu) kilugha, huwa lina maana ya kule mtu kukaa na kubaki katika sehemu au pahala maalumu, huku akiwa ameshikamana na jambo maalumu ndani ya mahala hapo, lakini neno hili kitaalamu (kwenye fani ya sheria za Kiislam) linamaanisha kule mtu kukaa katika sehemu takatifu kwa ajili ya ...
Neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر), humaanisha utafutaji wa hila au njia katika kulifikia jambo fulani, na yawezekana mtu kutafuta hila na njia za kuyafikia mazuri au mabaya. Ujanja wa Mungu: kuna Aya tofauti ambazo zimeliegemeza na kulinasibisha neno (ujanja مکر) ...