advanced Search
KAGUA
12862
Tarehe ya kuingizwa: 2018/11/11
Summary Maswali
Vipi talaka hutimia, maneno gani hutumika kwa ajili ya talaka, na ni mara ngapi?
SWALI
Vipi talaka hutimia, maneno gani hutumika kwa ajili ya talaka, na ni mara ngapi?
MUKHTASARI WA JAWABU
Kulingana na madhehebu ya Shia, iwapo mtu atakasirika kupita budi, kiasi ya kwamba akawa ametoa talaka bila ya makusudia au bila ya hiari kwa kutokana na kutawaliwa na hasira kupita budi. Hapo talaka haitakutimia. Ila kama atakuwa amekasirika kupitia budi, ila bado yupo timamu na akawa ametoa talaka kwa makusudio kamili na kwa hiari yake, basi talaka itakuwa imetimia.
Jawabu ya swali lako utaipata kupitia namba maalimu inayohusiana na swali lako.
Baadi ya madhehebu ya Kiislamu, yamelilainisha mno suala la talaka limepewa njia nyepesi kupita budi katika ukubalikaji wake, jambo ambalo limesababisha katika zama zetu hizi suala la talaka kuonenaka ni kama mchezo tu. Ama kwa upande wa madhehemu ya Shia, suala hili linaangaliwa kupitia ngazi tofauti katika kupokelewa na kukubalika kwake. Kishia talaka ni hukumu yenye toleo la upande mmoja, yaani mume ndiye mwenye haki ya kutoa talaka. Wakati wowote ule mume anaweza kumuacha mkewe kupitia mfumo ufuatao:
    Talaka ni lazima isomwe kwa lugha ya Kiarabu kupitia ibara maalumu kma vile «زَوْجَتِى فٰاطِمَةُ طالِقٌ» yaani mke wangu Fatuma ameshaachika, na iwapo atamuwakilisha mtu kumwacha mkewe, basi wakili huyo atasema «زَوْجَةُ مُوکِّلى فٰاطِمَةُ طٰالِقٌ» yaani mke wa mwakilishwa wangu ambaye ni bibi Fatuma ameshaachika.
   Ili talaka itimie ni lazima zizingatiwe sharti zifuatazo:
1- Mwachaji (mume) ni lazima awe ni mwenye akili timamu, na mwachaji kuwa ni baleghe pia ni sisitizo la wajibu. Pia awe hakulazimishwa bali kaacha kwa hiari yake, na iwapo atakuwa amelazimishwa amwache mkewe, talaka hiyo haitosihi.
2- Mtoaji talaka awe amekusudia kutaliki, kwa hiyo kama ataisoma ibara ya talaka kimchezo (kiutani), talaka hiyo haitosihi.
3- Anayeachwa awe yupo tohara, yaani asiwe katika hali ya hedhi au nifsi, na mumewe awe hajamuingilia (hajatenda naye tendo la ndoa) ndani ya tohara hiyo. Yaani awe bado hajawahi kumuingilia baada ya kutoharika, la ikiwa amemuingilia, basi itambidi asubiri hadi aingie katika hedhi kwa mara nyengine kisha atoharike, baada ya kutoharika asije kumuingilia, hapo ndipo anaweza kumpa talaka.
Ila kuna sura tatu ambazo yawezekana mke kutalikika (kuachika) huku akiwa ndani ya hedhi au nifasi;
A- Mume baada ya kuoana na mke huyo awe hajawahi kutenda naye tendo la ndoa ambalo limetimia, yaani kukutana kwa tupu mbili ambapo sehemu ya matahiriyo ikawa imezama katika tupu ya mwanamke.
B- Iwapo mke atakua na mimba, katika ambayo mume atakuwa amemuacha mkewe huku akiwa na hedhi, katika hali ya kuto kujua kuwa ana mimba, kisha tena baadaye akafahamu kuwa yeye alipomuacha alikuwa katika hali ya ujauzito, basi talaka itakuwa imefaa.
C- Iwapo mume atakuwa yupo mbali na ikawa ni vigumu (hakuna uwezekano) yeye kufahamu kuwa mkewe yupo ndani ya hedhi au ameshatoharika. Hapo talaka itasihi.
4- Iwapo mume atamuoa mwanamke, kisha akamuacha kabla ya kutenda naye tendo la ndoa. Hapo mume atawajibika kumpa mwanamke huyo nusu ya mahari waliyokubaliana hapo mwanzo walipomuoana. Ama akiwa tayari ameshatenda naye tendo la ndoa, basi ni wajibu wa mume kumlipa mwanamke huyo mahari yake kalimi.
5- Iwapo tamko la talaka litatoka mara moja na shuruti zake zikawa zimekamilika, basi hakuna haja kurudia tena ibara hiyo kwa mara ya pili. Na kwa mara hiyo hiyo moja talaka itakuwa imeshatoka na kukamilika na mke atakuwa tayari ameshaachika. Iwapo mke na mume wataachana   mara mbili kisha wakarudiana, iwapo atamuacha tena mara ya tatu, hapo haitokubalika wao kurudiana. Na mke atakuwa ni haramu kudiwa tena na mume huyo. Ila kama mke huyo baada ya kumalizika eda ataolewa na mume mwengine kisha akaachwa, hapo mume wa mwanzo anaweza kumuowa tena mke huyo baaya kwishwa eda yake. Pia ni lazima huyo mume ambaye atamuowa baada ya lalaka hiyo ya tatu, ni lazima awe ni baleghe na mwenye aliki timamu, na vile vile ni lazima amuingilie na awe amemuoa kwa nia ya kuishi naye ndoa ya daima. Pia yawezekana ikaulizwa je hivi inajuzu katika kikao kimoja mume akatoa talaka moja kisha hapo hapo akamrudia mkewe hali mke akiwa hayupo kikaoni, kisha akamuacha tena papo hapo. Je talaka ya aina kama hii itajuzu? Wanazuoni wamekhtalifiana juu ya jambo hili. Wenge wansema yawezekana, na wengine amekataa. Waliosema yawezekana wamedai kuwa si lazima katika kumrudia mke kupite tendo la ndoa au mke awepo katika kurudiwa huko, ila kama sharti za talaka zitatimia basi talaka itakuwa imesihi.
6- Iwapo mke ataachika basi ni lazima asubiri hadi apitiwe na hedhi mbili na tohara mbili, na atakapoingia katika hedhi ya tatu, hapo eda itakuwa imemalizika, na aweza kuolewa tena. Na iwapo mwanamke atakuwa haingii katika hedhi lakini umri wake ni wa kuingia hedhi, kisha akaachwa, basi katika hali hiyo ya yeye kutoona hedhi (pengone ni mgonjwa), eda yake itakuwa ni miezi mitatu. Eda ya ya mtu mwenye mimba ni hadi kujifungua, akijifungua tu eda itakuwa imemalizika. Au iwapo ataharibu, yaani mimba yake ikaharibika na mtoto akatoka kambla ya muda, pia yeye eda yake itakuwa ni baada ya kuharibika kwa mimba hiyo.
Ama kuhusiana na ndoa ya muda (mut’a) ambayo ni yenye kukubalika katika madhehebu ya shia, talaka ya ndoa hii baada ya kumalizika muda waliyokubaliana, au mume kusamehe muda uliobakia. Na eda yake ni hedhi mbili, yaani baada ya mwanamke kuungia katika hedhi mara mbili na kutohariaka. Na kwa wale wasioona hedhi eda yao ni siku 45.
 
Kwa hiyo kuhusiana na kupita talaka kwa sms, hapo yatupasa kuangalia hali na sharti za talaka tulizokufafanulia katika makala hii. Lakini kwa kukusaidia tu ni kwamba; iwapo yeye atamuakilisha mtu amtaliki mkewe, kisha pia wakawepo mashahidi adilifu katika kuishuhudia talaka hiyo. Hapo bila shaka talaka itasihi, na wala hapatakuwa na pingamizi juu yahilo.
 
 
TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI