Please Wait
KAGUA
13878
13878
Tarehe ya kuingizwa:
2006/08/27
KODI YA TOVUTI
fa399
NAMBARI YA HIFADHI
51515
- Shiriki
Summary Maswali
nini siri hasa ya Uslamu kuwa ni dini ya mwisho, na nini pingamizi hasa ya bwana Surush juu ya hilo?
SWALI
Swali liloulizwa hapo juu, linatokana na mtazamo maalumu wa Bwana Surush kuhusiana na kule Uislamu kuwa ni hitimisho la dini, mtazamo ambao umeweza kushawishi na kuzikanganya akili za baadhi ya vijana. Pingamizi zinajibiwa makalani humu kuhusiana na jambo hili, ni kama ifuatavyo:
Dini za mbinguni zilionekana kubadilika kimaendeleo kutoka zama moja hadi nyengine, na sababu hasa ya kupatikana maendeleo na mabadiliko hayo, ni kule jamii ya wanadamu kutanuka kifikra na kimaendeleo. Pia dini ya Kiislamu nayo haikuweza kuepukana na hali hiyo ya mabadiliko ndani yake, na hii inatokana na jamii ya wanadamu wa zama za leo kuwa na maendeleo zaidi kuliko wanadamu wa zama nyengine zilizopita. Jamii ya leo ni yenye kubadilika kwa haraka mno kimaendeleo, wala huwezi kuilinganisha na ile jamii ya Waislamu wa mwanzo waliopita kabla yetu. Kanuni za ibada zaweza kubaki bila ya mabadilko; kwani kanuni hizo ni zenye mahusiano ya moja kwa moja na Mungu mwenyewe, na wala hazina uhusiano wowote ule na hali ya mabadiliko ya zama au upanukaji wa akili za wanadamu. Ama kanuni na sheria za kijamii na kiserikali, hazitokosa kuwa na haja ya mabadiliko na kufanyiwa ukarabati ndani yake.
Kule dini ya Kiislamu kuhisabiwa kuwa ni dini ya mwisho; hakumaanishi kuwa sheria zake ni sheria zisizokubali mabadiliko ndani yake, bali ni kwa sababu ya wanadamu kuto hitajia dini nyengine mpya kutoka mbinguni. Kwa maana hiyo; dini ya Kiislamu yaweza kumshika mwanadamu mkono na kumfikisha malengoni. Hiyo inamaanisha kuwa; dini yaweza kumuongoza mwanadamu katika uvumbuzi wa kanuni za Kiisamu, ziendazo sawa na hali ya mazingira ya wanadamu yalivyo katika zama mbali mbali. Na hii ndiyo maana halisi ya dini ya Kiislamu kuitwa dini ya mwisho.
MUKHTASARI WA JAWABU
Kuzingatia nukta zifuatazo kutaweza kumsaidia msomaji kulitambua vyema suala hili:
1- Hitimisho la utume lina maana ya hitimisho la dini; na hii inamaanisha kuwa hakutokuja mtume mwengine baada Yake (s.a.w.w). Hayo pia utayakuta kwenye Aya ya 40 ya Suratul-Ahzab.
2- Dini ya Kiislamu imeitwa dini ya mwisho kwa sababu zifuatayo:
A- Ukamilifu wa Uislamu; yaani si kwa upande wa mtangazaji au msambazaji wa dini hiyo kuwa aliwekewa mipaka ya kiwango maalumu cha mafunzo katika utangazaji wake, na wala hakukuwa na mipaka maalumu ya rangi, kabila, nchi n.k. juu ya walengwa wa dini hiyo. Kwa hiyo dini ilikisema na kukibainisha kila kinachohitajiwa na wanadamu kibaga unaga.
B- Kutochafuliwa kwa kitabu cha Mola Mtukufu (Qur-an).
3- Dini ya Kiislamu ina sheria na kanuni thabiti za kudumu, pia sheria na kanuni za mpito. Uislamu kupitia maimamu (Ahlul-Bait a.s) ulikwisha weka mfumo imara wa uchambuzi na utofautishaji wa aina mbili hizo za sheria na kanuni. Mfumo ambao hujulikana kwa jina la (ijitihadi), nawo ndiyo njia pekee muwafaka ya utatuzi wa matatizo ya kijamii na kibinafsi. Kushikamana na mfumo huu wa ijitihadi pamoja na Qur-ani tukufu, ndiko kulikoifanya dini ya mwisho kuwa ni dini kamili na madhubuti.
4- Utafiti wa kidini kupitia njia ya ijitihadi, wenye nia ya kupata ufumbuzi na kuifikia falsafa ya sheria za Kiislamu; hauwezi kudhuriwa na maendeleo ya elimu za sayansi na jamii. Kwa upande mwengine; elimu za sayansi na jamii zaweza kutoa mchango mkubwa wa ufanisi kwa wanazuoni, pamoja na kuwapa wao uoni mkubwa zaidi utakaowasaidia wawe makini zaidi katika aina mbali mbali za tafiti zao za kidini. Na siyo elimu na sayansi ziwe ndiyo sababu za kuzifanya sheria za kudumu kuwa ni za mpito, hasa tukizingatia kuwa; sheria nyingi za kijamii na kisiasa za Kiislamu, ni sheria za kudumu.
5- Madai ya bwana Surushi kuhusiana na suala hili; ni madai yasiyokuwa na dalili, hii ni kwa upande mmoja, na kuwa upande mwengine ni kwamba; madai haya ya bwana Surushi ni yenye kukabiliwa na vikwazo mbali mbali. Maoni ya bwana Surushi yanazihisabu sheria na kanuni za kidini kuwa ni kanuni za kuzuka kiholela kuendana na matokeo ya kijamii na wanajamii wenyewe walivyo. Maoni yake ni yenye kwenda sambamba na mfumo wa secularism, hii inatokana na yeye kukosa mtazamo sahihi juu ya dini hii ya Kiislamu.

JAWABU KWA UFAFANUZI
Kwanza kabisa yapasa kufahamu kuwa;
1- Waislamu waote kwa jumla -pamoja na tofauti zao za kimadhehebu walizonazo- wanaamini kuwa dini ya Kiislamu ni dini ya mwisho. Mola Hakimu katika Qurani tukufu anasema; "Muhammad (s.a.w.w) si baba wa yeyote yule miongoni mwa wanaume wenu, bali ni mtume wa Mwenye Ezi Mungu na ni mtume wa mwisho, na Mwenye Ezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu". Neno mwisho ambalo kwa lugha ya Kiarabu ni (خاتم), linamaanisha ukomo na hitimisho, au pia neno hili huwa na maana ya nyenzo ya kupigia muhuri kwenye nyaraka mbali mbali. Nyenzo ya kupigia muhuri imeitwa (خاتم) kwa kutokana na kule nyenzo hiyo kuwa ndiyo nyenzo ya kuhitimishia maandiko maalumu, ipigwayo mwishoni mwa maandiko mali mbali. Pete nayo pia kwa lugha ya Kiarabu huitwa khatam (خاتم). Imeitwa hivyo kwa sababu ya pete kutumika kama ni nyenzo ya kupigia mihuri katika zama zilizopita, au hata za hivi karibuni. Maana halisi basi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuitwa (خاتم); inatokana na kuwa yeye ndiye hitimisho la mitume, na wala hakutakuja mtime mwengine baada yake (s.a.w.w). Baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu wamelifasiri neno (خاتم) kuwa ni; Mtume aliyetimiza hatua zote ujumbe wa Mola, yaani amewamiminia watu kila kinachohitajika bila ya kubakisha kitu, huku yeye mwenyewe pia akiwa ni mwenye aina zote za ukamilifu kushinda wanadamu wote.
2- Kumefanyika tafiti mbali mbali kupitia wanazuoni wa Kiisalmu kuhusiana na siri na maana halisi ya suala hili la hitimisho (خاتمیه).
Sisi tunaamini ya kwamba; binadamu ni kiumbe mwenye hisia za kimaumbile zenye kiu ya kumtafuta Mungu au muabudiwa. Lakini hii haimaanishi kuwa; kila itikadi atakayoshikamana nayo mwanadamu kuwa ni itikadi sahihi, kwani hisia hizi za kimaumbile hazitoshi kuwa ndiyo ramani kamili ya kumuongoza yeye katika njia sahihi. Bali hali hii ya kimaumbile aliyokuwa nayo, bado itahitajia uoni makini utakaomuongoza katika njia ya haki. Mola Mtukufu amempa mwanadamu akili ambayo huwa ni mtume aliyemo ndani ya kila mwanadamu, pia akamuengezea mjumbe mwengine wa nje (mitume) wa kumsaidia yeye katika yale ashindwayo kuyafikia ufumbuzi wake kupitia akili yake hiyo ya kibinadamu iliyo na mipaka maalumu.
Hivyo basi mitume wamekuja kumuongoza mwanadamu katika njia salama ya uongofu, na kila dini ilipokuja ilifinywa na mabano mawili; kiwango maalumu cha mafunzo ya Wahyi wanayoyapokea mitume kwa ajili ya walengwa wao, na kiwango maalumu cha uwezo wa akili za wanajamii katika ufahamu wa kuyaelewa mafunzo ya Wahyi huo, jamba ambalo pia limepelekea kupatikana kwa upotoshwaji wa Wahyi ndani ya zama mbali mbali. Sababu hasa iliyopelekea kuletwa matoleo mapya ya dini katika zama mbali mbali, ni kule jamii za wanadamu kutaalamika na kukua kiakili kutoka zama moja hadi nyengine. Na kila toleo jipya lilipokuja liliyasawazisha machafuzi yaliyofanya na wadadamu waliopita, pamoja na kuikamilisha dini ilipita kabla yake, suala hili liliendelea hadi ilipokuja dini ya mwisho (ya Kiislamu).
Dini ya Kiislamu haikua kwenye aina yeyote ile ya mabano na mipaka au vizuizi vilivyozifinya dini zilizokuja kabla yake; yaani mtume wake alipikika kisawasawa kwa kule yeye (s.a.w.w) kuteremshiwa mafunzo kamili kwa ajili ya wanadamu wote wa zama zake na zijazo, pia walengwa wake ni wenye ufahamu wa hali ya juu kabisa ukilinganisha na walengwa wa dini zilizopita kabla yake. Umakini wa kiakili wa wafuasi wa dini hii pia umekuwa ndiyo ngao iilindayo dini hii kutokana na aina mbali mbali za machafuzi; hii inamaanisha kuwa haidhuru si watu wote ni wenye uwezo mkubwa wa kiakili, lakini bado kuna wengi wenye uwezo mkubwa mno wa kiakili katika umma huu. Hao basi ndiyo ngao makini iilindayo dini ya Mola Mtukufu. Kuto kuweo kwa vizingiti tulivyovitaja vilivyozikanza dini zilizopita kabla yake, ndiko kulikoiwezesha dini hii kutoa mafunzo kamili kwa wanadamu wote kwa jumla. Pia baadhi ya mafunzo yaliyokuja kwenye dini hayakuwa ni mageni, kwani pia mafunzo hayo yalionekana kufunzwa na dini zilizokuja kabla yake. Kule dini hii kukusanya mafunzo yaiyopita na yajayo pia kumechangia kuifanya dini hii iwe ni dini kamili iliyohitimisha dini zote zilizokuja kabla yake.
Ili dini iwe ni kamili; ni lazima na ulinzi kamili wa kuilinda na machafuzi mbali mbali. Uislamu nao umelindika na hilo kupitia ngao mbili zifuatazo;
A- Ngao ya Qur-ani isiyotilika mkono kwa njia yeyote ile.
B- Fomula (njia na mfumo) maalumu uliotayarishwa na dini kwa ajili ya kuyafahamu mafunzo yake; kuwepo kwa mfumo na njia maalumu inayomuwezesha mwenye ujuzi nayo kuyafikia mafunzo halisi ya uislamu, kumeifanya dini hii iwe ni dini isiyoyumba.
Dini za mbinguni - kama asemavyo Shahid Mutahari - ni kwamba; zimejengeka kupitia kanuni za daima na za mpito. Kanuni za daima ni kama vile sehemu asili za maumbile ya binadamu zilivyo si zenye kubadilika, nazo siku zote hubaki thabiti bila ya mabadiliko, na zaendana sawa na zile sehemu msingi za maumbile alizonazo mwanadamu. Na kwa upande mwengine dini haijaifumbia jicho ile sehemu ya pili ya maumbile ya mwanadamu yenye mabadiliko ya mara kwa mara. Kulingana hali hii ya pili ya kimaumbile aliyonayo kila mwanadamu, dini ilizitayarisha kanuni maalumu za mpito zenye kukubali mabadiliko kuendana na zama pamoja na mahala alipo kiumbe huyu. Sheria zote mbili za mpito na daima; zimo katika kasha maalumu la sheria kutoka mbinguni, na funguo za kulifungua kasha hilo kwa ajili kuzitambulisha kanuni za daima na za mpito katika hali na zama mbali mbali, zimewafikia wanazuoni wetu kutoka kwa Ahlul-Bait (a.s). Njia hii ya kuwepo wanazuoni wenye uwezo wa kuwafafanuliwa watu sheria zinazowahusu wao binafsi pamoja na jamii zao, ni njia itoshelezayo jamii zote katika zama ambazo jamii hukanzwa na matatizo mbali mbali ya kuifikia miongozo salama ya kisheria na kijamii.
Ni wazi kwamba ongezeko kubwa la kanuni na sheria za kifiqhi katika zama za hivi sasa; linatokana na kuengezeka kwa mahitajio ya wanajamii wa kileo. ongezeko ambalo limekuja kutokana na maendeleo ya elimu mbali mbali kuongezeka kupita budi. Pia ni wazi kabisa kwamba; sheria za daima itabidi kubaki kuwa ni za daima, na dini imetoa mfumo na njia maalumu za kuyatatua matatizo kuhusiana na mahitajio ya wanadamu katika zama tofauti. Jambo ambalo limeitosheleza dini hii na kuifanya kuto kutajia mtume mwengine wa kutuletea dini nyengine mpya.
Ili suala zima la kuja kwa mitume mbali mbali waliotoa mafunzo ya hatua kwa hatua hadi kufikia dini hii kamili liweze kufahamika, inabidi kutoa mfano ufuatao:
Jaalia jamii ya wanadamu ni kama wanafunzi wa skuli wanaojifunza hesabati; ili wanafunzi hawa waweze kufahamu vyema, ni lazima wasomeshwe hatua kwa hatua kupitia viwango na walimu tofauti kulingana na viwango uwezo wao. Pale wanafunzi hawa wanapofikia kiwango maalumu, hufunzwa na kupewa formula maalumu zitakazowawezesha kupata ufumbuzi wa aina mbali mbali za matatizo ya fani ya hesabati maishani mwao. Lakini hilo halitowafanya wao wadai kuwa; hawana haja tena ya mafunzo waliyoyapata shuleni, kwani mafunzo hayo ndiyo msingi wa yote yale waliyoyachuma baada yake. Na wala wao hawatoweza kuitupilia mbali ile misingi mikuu minne ya hesabati waliyoisoma utotoni mwao; yaani kutoa, kujumlisha, kuzidisha na kugawa (- + × ÷) kisha wadai kuanzisha misingi yao mipya, kwani jambo hilo halitawezekana na liko nje ya uwezo wao.
3- Mtazamo wa Dr. Surushi kuhusiana na hitimisho la dini; si mtazamo mpya juu ya hilo. Lakini chimbuko hasa la mtazamo wake huo linatikana na jawabu ya Iqbali Lahuri juu ya swali lisemalo; je kuna fungamano lolote juu ya kukamilika kwa dini fulani na hali ya tamaduni na maendeleo ya kielimu ya zama za kuteremka kwa dini hiyo? Jawabu ya Dr. Surushi ni sawa na jawabu ya Iqbali Lahuri, isipokuwa tu yeye (Dr. Surushi) ameifuma tena jawabu hiyo kwa mfumo mwengine mpya. Jawabu ya Dr. Surushi juu ya swali hili ni kwamba; jamii ya wanadamu itaendelea kielimu na kukua kiakili siku hadi siku mpaka itafikia wakati ijitosheleze na isihitajie tena dini. Au kwa lugha nyengine tuseme kwamba; mafunzo ya mtume (s.a.w.w) ni mapana yenye upeo wa juu mno, kiasi ya kwamba yamekuwa ni toshelezo kwa zama zote, na hakuna haja tena ya kuja mtume mwengine. Yaani ni kama vile mwanafunzi anapofikia kiwango cha kutohitaji mwalimu wa kumpa miongozo kwa kutokana na yeye kufikia kiwango mwalimu.
Kwa mtazamo wa mwanazuoni ajulikanaye kwa jina la Iqbali Lahuri ni kwamba; kama ilivyo kawaida, viumba katika hatua ya kwanza ya kimaumbile huwa ni wenye kutegemea miongozo ya kimaumbile walionayo. Na hatimaye hatua kwa hatua hisia, fikra na akili zao hukua na miongozo yao ya kimaumbile hupunguka nguvu. Wanadamu wanaoishi katika ulimwengu wa hivi sasa, tayari wameshaziweka nyuma zile hatua za kimaumbile walizokuwa nazo utotoni mwao, hivyo basi wao hawana haja tena ya Wahyi. Kwa mtazamo wake yeye ni kwamba; itafikia zama fulani watu wawe hawana haja tena dini, na hiyo ndiyo sababu ya kuhitimishwa kwa dini hii.
Wanaitikadi wa Kimarxist (Marxists) ni miongoni mwa Walahidi wenye mtazamo ufananao na wa Iqbali Lahuri. Wao wanaona kuwa; sifa maalumu walizokuwa nazo Waislamu wa mwanzo na Waislamu waliokuja baada yao, ndiyo sababu hasa ya kuhitimishwa kwa dini. Wao wanasema kuwa; dalili ya mtume (s.a.w.w) kuitangaza dini hii kuwa ni dini ya mwisho, inatokana na uhodari na umahiri wake uliomfanya yeye kufahamu kuwa; muda si mrefu watu watalikunja jamvi la dini kwa kutokana na wao kuja funukia upeo mpya wa kielimu ulioko mbele yao.
4- Ni wazi kwamba maoni haya hayatoacha kukanzwa na vikwazo mbali mbali; na moja kati ya vikwazo hivyo ni usemi wa Shahidi Mutahari. Yeye kuhusiana na hili amejibu kwa kusema; maoni haya yanamaanisha kupatikana kwa hitimisho la dini, na sio hitimisho la utume. Hata hivyo; iwapo sisi tutakubaliana na maoni ya Dr. Surushi kama alivyofafanua kuhusiana na hili, tutalazimika kuamini ya kwamba; siku hadi siku ni lazima watu wawe wanaendelea kuufahamu Uislamu halisi na kuingia ndani yake, hali ya kwamba haionekani hali hiyo kuwa ni sahihi. Pia itatubidi kuamini kuwa misingi yote ya dini pamoja na uchambuzi wake kama vile; maana ya dini, kazi za dini, malengo ya dini, malengo ya kuja mitume, utando wa dini, huduma za dini katika nyanja mbali mbali za jamii, pamoja kazi za dini za kutafuta ufumbuzi mbali mbali wa matatizo ya jamii, yote hayo yawe yamebadilika kabisa kabisa. Pia itabidi tuseme kuwa; dini ni kinyume dalili za kihistoria zilivyo, haikuja kuwaongoza watu katika mafanikio ya Akhera na duni, bali imekuja kuwapa wao miono ya kuishi kidunia tu. Hivyo itapelekea dini kuwa si kamili, na mafunzo yake yatakuwa ni ya mpito tu, na jinsi ya utambuzi wa binadamu unavyotanuka na sheria nazo pia zitazidi kuwa nyingi zenye rangi mbali mbali, na wala hatutakuwa na sheria thabiti. Nayo pia itapelekea kuamini kuwepo kwa mfinyiko na mkunjuko wa sheria. Jambo ambalo si lenye kukubalika na hii inatokana na kuwepo kwa dalili na hoja nyingi katika kupingana na mtazamo wa aina kama hiyo. Na kule kukwaruzika kwa mtazamo huu juu suala la hitimisho, litapelekea vile vile kutingatinga kwa kwa mtazamo wa Dr. Surushi juu ya hilo.
Hapa sasa tumeshaona ya kwamba; kuhitimika na kukamilika kwa dini hii, kutokanako na kuto kuwepo kwa mipaka kwa upande wa walengwa wake, haimaanishi kuwa watu wote watakuwa wameufikia uwezo na upeo wa juu kabisa wa kiakili katika kuyaelewa mafunzo ya dini. Lakini hilo linamaanisha kuwepo kwa baadhi ya waliokuwa na uwezo mkubwa wa ufahamu unaowawezesha wao kuyahifadhi mafunzo ya dini yao. Kwa lugha nyengine ni kwamba; kuna fungamano muhimu baina ya dini hii ya mwisho na mazingira ya kijamii, kitamaduni na kielimu ya walengwa au wafuasi wa mwanzo wa dini hii na wanaofuatia. Yaani kulindika na kuhifadhika kwa dini hii, kutokana na kuwepo baadhi ya watu walioweza kukifikia kiini halisi cha dini, kisha wakawarithisha wengine mafunzo ya dini hiyo. Na sio kwamba kuna wakati fulani, watu wote wataifahamu dini kisawa sawa; kiasi ya kwamba wasiwe na haja tena ya kupata mafunzo ya kidini, au hata bila ya wao wenyewe kujitambua wawe ni walinzi na wahifadhi wa dini hiyo.
5- Kama ilivyofafanuliwa hapo mwanzo ya kwamba; dini ni yenye nguzo mbili muhimu, nazo ni sheria za kudumu na za mpito. Na kwa upande wa pili tuna maendeleo ya kieimu katika zama tofauti, lakini hakuna aiana yoyote ile ya mgongano baina ya maendeleo hayo na nguzo mbili hizo. Hii ni kwa sababu; maendeleo ya kielimu hutusaidia sisi kuwa na mtazamo mpana zaidi katika kutafuta hukumu na sheria muwafaka juu ya jambo fulani. Na uamshaji au usinduzi wa sheria fulani za kiserikali au kijamii -ziwe za mpito au za daima-, huzinduliwa kupitia misingi mikuu ya kifiqhi (formula). Kwa hiyo ukweli kabisa ni kwamba; maendeleo ya kielimu hutusaidia sisi kupata njia muwafaka za kuzifanyia kazi sheria zinazozinduliwa na formula hizo za kifiqhi. Na wala isidhaniwe kuwa sheria zote za kijamii au za kiserikali kutoka zama moja kwenda nyengine huwa ni za mpito tu, bali bado kuna sheri nyingi ndani yake huwa ni za kudumu, na kuzifikia sheri hizo za kudumu ndiko kutakoweza sisi kuitambua falsafa ya dini pamoja na kutupa muelekeo katika nyanja maalumu; kama vile: nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Twataraji wahakiki wetu wa kidini na kijamii watafaidika na makala hii. Kama kuna suali lolote kuhusu makala hii, tuulize kupitia tovuti yetu; www.islamquest.com.

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI