advanced Search
KAGUA
11557
Tarehe ya kuingizwa: 2010/08/08
Summary Maswali
nini hukumu ya mtu aliyekuwa anadaiwa funga kisha akawa hakuilipa funga hiyo hadi akafikiwa na Ramadhani nyengine ya mwaka ulioufata?
SWALI
napenda kujua nini hukumu ya mtu aliyekuwa hakulipa deni la funga ya mwaka uliopita hadi akafikiwa na Ramadhani nyengine?
MUKHTASARI WA JAWABU

Tokeo hilo linaweza kutokea katika sura tatu, nasi tutazifafanua sura hizo na kuzijibu kwa mujibu mitazamo ya maulamaa isemavyo. Na jawabu zetu ni kama ifuatavyo:

1- iwapo mtu ataacha kufunga kwa kutokana na maradhi, kisha maradhi hayo yakaendelea hadi akafikiwa na Ramadhani ya mwaka wa pili, mtu huyo hatowajibikiwa kuzilipa funga hizo, bali atatakiwa kuzilipia fidia, na kiwango cha fidia hiyo kwa kila siku moja ni gramu 750 za ngano, mchele au kinachofanana na hivyo, na fidia hiyo inatakiwa kupewa mafakiri, lakini ni vizuri kutoa gramu 1500 kwa kila siku moja iliyompita.[1]

2- iwapo mtu atakuwa haweza kuzilipa funga hizo kwa udhuru mwengine, kama vile kuwa safarini, kisha udhuru huo akabaki nao hadi akaingiliwa na Ramadhani ya mwaka wa pili, huyo atatakiwa kuzilipa funga hizo na pia ni vizuri kuzilipa kwa kuzifunga na kuzilipia fidia, yote mawili kwa pamoja, na fidia hiyo ni kumpa fakiri gramu 750 za chakula kilichotajwa katika suala namba moja kwa kila siku moja.[2]

3- iwapo mtu ataacha kufunga kwa kutokana na udhuru fulani, kisha udhuru huo ukamuondokea baada ya kwisha Ramadhani, lakini yeye kwa makusudi akaacha kuzilipa funga hizo hadi kufikia Ramadhani nyengine, yeye atatakiwa kuzilipa funga hizo kwa kuzifunga, pia atatakiwa kuilipia kila siku moja kiwango cha gramu 750 za chakula na kumpa fakiri au mafakiri iwapo kiwango cha fidia hizo zitakuwa ni zaidi ya chakula cha fakiri mmoja.[3]

 


[1] Sherehe ya imam Khomeiniy  Taudhihul-masaaili, juz/1, uk/947, suala la 1703.

[2] Sherehe ya imam Khomeiniy  Taudhihul-masaaili, juz/1, uk/947, suala la 1703.

[3] Sherehe ya imam Khomeiniy  Taudhihul-masaaili, juz/1, uk/947, suala la 1705.

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

 • nini maana ya itikafu
  16322 اعتکاف
  Neno (itikafu) kilugha, huwa lina maana ya kule mtu kukaa na kubaki katika sehemu au pahala maalumu, huku akiwa ameshikamana na jambo maalumu ndani ya mahala hapo, lakini neno hili kitaalamu (kwenye fani ya sheria za Kiislam) linamaanisha kule mtu kukaa katika sehemu takatifu kwa ajili ya ...
 • iwapo mtu ndani ya usiku wa mwezi wa Ramadhani atabakia na janaba hadi wakati wa adhana ya asubuhi kwa makusudi bila ya kukoga, mtu huyo atatakiwa kufanya nini? Je ailipe ile siku moja tu, au pia atatakiwa kulipa fidia?
  18847 قضای روزه و کفارات
  iwapo mtu atawajibikiwa kufunga mwezi wa Ramadhani, naye kwa makusudi akabakia na janaba hadi adhana ya asubuhi, anaweza yeye akatayamamu katika nyakati za mwisho kabisa kabla ya kuadhiniwa adhana hiyo badala ya kuoga, kwa kuwa wakati wa kuoga haupo tena, kisha aendelee na funga yake, na funga ...
 • nini hukumu ya kufuga njiwa ndani ya sheria za Kiislamu? Na nini msingi hasa wa hukumu hiyo?
  21320 نگهداری و شکار حیوانات
  Tukilitazama suala la kufunga njiwa kibinafsi, tutalikutia kuwa suala hili halina matatizo na ni halali. Lakini pale sisi tutapolimbatanisha suala hili na haki za majirani au wanajamii, hapo tunaweza kulipa picha ya uhalali au uharamu kwa jinsi hali za jamii mbali mbali zinavyolitazama suala hilo. Baadhi ya ...
 • je mtu asiwajibikiwa kufunga (asiyefunga) ana ulazima wa kutoa zakatul-fitri?
  9386 زکات فطره
  Mtu atakaeingiliwa na usiku wa Idil-fitri, huku akiwa ni baleghe na mwenye akili timamu, naye akiwa si mtumwa wa mtu wala si fakiri, mtu huyo atawajibika kutoa zakatul-fitri kwa ajili yake na kwa ajili ya wale wote anaowahudumia, na kiwango cha kila mmoja ni kiasi cha kilo ...
 • Vipi mtu anaweza kuwa kipenzi cha Mwenye Ezi Mungu?
  4595 Tabia kimatendo
  Katika lugha ya Kiarabu, -ambayo ndiyo lugha ya sheria ya Kiislamu- neno (pendo) linatokana na neno "حب". Ambalo lina maana ya kule mtu kuwa na mapenzi na mtu, kitu au jambo fulani. Lakini neno pendo, mapenzi au neno jengine lenye maana kama hii, linapotumika na kunasibishwa ...
 • nini ilikuwa hatima ya farasi wa Imamu Husein (a.s) huko Karbala?
  6286 حوادث روز عاشورا
  Waandishi mbali mbali wa walioandika na kulizungumzia tokeo la Karbala, hawakutoa ufafanuzi wa kutosha kuhusiana na farasi wa Imamu Husein (a.s), bali walichokielezea ni kuwa, farasi huyu alijipakaa damu ya Imamu Husein (a.s), kisha akaelekea kwenye mahema huku akitoa sauti kali yenye kuashiria huzuni na hasira. Watu ...
 • nini maana ya ucha Mungu?
  16503 تقوی
  Taqwa (ucha Mungu) ni nguvu maalumu za kiroho zinazo weza kupatikana ndani ya nafsi ya mwanaadamu, nguvu ambazo huwa ni himaya maalumu inayomuwezesha yeye kujitenga na maasi. Taqwa kamili ni ile inayomfanya mtu kujiepusha na maasi yanayo eleweka na kila mmoja wetu, pamoja na kujiepusha na yale ...
 • je ni kweli kuwa Imamu Hsein (a.s) alifunga ndoa na bibi Shahre-Baanu?
  7825 امام حسین قبل از امامت
  Suala la ndoa ya Imamu Husein (a.s) na bibi Shahre Baanu aliyetekwa na jeshi la Kiisalamu, ni suala liliozungumziwa na vitabu vya historia huku likiwa na rangi mbali mbali za Ibara zenye kutofautiana, baadhi ya kauli zimesema kuwa: yeye alitekwa katika zama za utawala wa Omar, huku ...
 • je dini na siasa ni vyenye kuendana au vyapingana?
  10560 Elimu mpya ya Akida
  Dini ni chombo maalumu kilichokuja kumkomboa mwanaadamu na kumuongoza katika njia ya mafanikio, hivyo basi ni jambo lisiloingia akilini kuwa chombo hichi kiwe ni chenye kulipa mgongo jambo muhimu linalohitajika ndani ya jamii mbali mbali, kama vile suala la usimamishaji wa serikali. Na kwa upande mwengine ni ...

YALIYOSOMWA ZAIDI