advanced Search
KAGUA
11914
Tarehe ya kuingizwa: 2012/05/05
Summary Maswali
maadili mema yana nafasi gani kwenye uwanja wa mazoezi?
SWALI
suala la maadili mema lina nafasi gani katika mambo ya mazoezi au katika uwanja wa michezo na mazoezi?
MUKHTASARI WA JAWABU

Uisalmu ni dini kamili iliyokusanya ndani yake mfumo kamili na salama wenye kutoa muelekeo wa kiutendaji kuhusiana na kipengele kimoja kimoja miongoni mwa vile vipengele vinavyo husiana na maisha ya mwanaadamu. Uislamu haukuliweka nyuma suala la afya ya mwili wa kila mmoja wetu. Kwa hiyo Uislamu ni wenye kuunga mkono sula la michezo na mazoeza mbali mbali yenye lengo la kuleta faida za kimwili na kiakili.

Hivyo basi, yale yote yenye kuzingatiwa miongoni mwa maadli mema ambayo yanamlazimu mwanaadamu kushikamana nayo ndani ya maisha yake ya kila siku, ni yenye ulazima wa kushughulikiwa na kutekelezwa ipaswavyo ndani ya maeneo ya michezo na mazoezi.

Miongoni mwa maadili mema yaliyo muhimu, ambayo mwana mazoezi anatakiwa kushikamana nayo, ni kupigana jihadi na nafsi yake katika kuto kwenda kinyume na maadili mema, pia yeye analazimika kushikamana na ubinaadamu pale aingiapo mashindanoni.

JAWABU KWA UFAFANUZI

Afya ya kimwili na kiroho, ni miongoni mwa mambo muhimu yanayo tiliwa mkazo na jamii mbali mbali za wanaadamu. Tukitambua kwamba: dini ya Kiislamu ni dini kamili, hivyo basi dini hii imewajibika kuja na sheria madhubuti itakayotoa mfumo kamili na maridadi wenye kuhusisha ndani yake zile nyanja zote zinazo fungamana na maisha ya kila siku ya mwanaadamu, mfumo ambao utakuwa ni wenye kutoa dhamana kalimi ya kumueka mwanaadamu katika maisha salama yenye amani na upendo, na pia jukumu hilo halitakiwi kuyalenga maisha ya Akhera au ya kidunia tu, bali ni wajibu wa Uislamu kuutandaza mfumo wake utakao yahusisha maisha ya duniani na Akhera kwa pamoja. Na kwa kutokana na kuwa: mazoezi, michezo na mashindano mbali mbali, ni moja kati ya mambo muhimu yasiyo wabanduka wanaadmu, pia  ni miongoni mwa yale yenye umuhimu wa afya za wanaadamu, hivyo basi Uislamu haukuliweka nyuma au kulipuuza suala hilo, bali  Uislamu ni wenye kulitilia mkazo kutokana na umuhimu uliyomo ndani yake.

 

  Leo ulimwenguni suala la michezo limekuwa ni miongoni mwa mambo yasio tengana na maisha ya kijamii. Mamilioni ya watu mabli mbali wamekuwa wakijishirikisha na suala hilo, pia sehemu kubwa ya wanajamii imeingia katika ushabiki wa kupenda na kushangiria michezo mbali mbali.

Michezo pia imeweza kutumika kuwa ni kama nyenzo muhimu ya kuleta umoja wa kitaifa na kizalendo. Iwapo basi ustaarabu na maadili mema utakuwa ni wenye kutupwa nyuma ndani ya suala hilo, jambo hilo litakuwa ni lenye kuashiria zile tamaduni mbovu zilizozagaa ndani ya jamii za wana michezo hao wa taifa fulani.[1]

 

   Maadili katika Nyanja za michezo na mazoezi, ni moja ya maudhui za fani ianayo husiana na maadili na ustaarabu mwema katika kazi na utendaji mbali mbali. Maudhui hii hulazimika kukabiliana na fikra na mitazamo tofauti ya kimaadili ndani ya nyanja za kisiasa, teknolojia, uongozi na nyenginezo, ili kuweza kupata suluhu na njia salama yenye maadili mema ya kiutendaji.[2] Kila mmoja miongoni mwa wanajamii huliangalia suala la michezo na mazoezi, kwa jinsi ya vile yeye anavyo liangalia suala hilo, mtazamo maridadi unaoweza kufikiriwa ndani ya suala hili ni ule usemao kuwa: michezo ni matendo ya kiufundi yenye nia ya kuuchangamsha mwili na akili kwa pamoja na kuvifanya viwe makini zaidi na tayari kwa kazi mbali mbali, hivyo basi sisi tunaweza kusema kuwa: michezo ni matendo yenye mfumo maalumu ambayo yamepangiwa kanuni madhubuti ndani ya jamii zetu zenye muelekeo mmoja kwa nia ya kuwaweka watu katika furaha, kufanya mashindano, kujichangamsha kibinafsi, kujidhatiti mbele za watu pamoja na kujiweka tayari kwa ajili ya maelengo na kazi mbali mbali.

    Ustaarabu na maadili mema juu ya suala hili, itabidi ufuatane na nia ya yule mwenye kufanya mazeozi.

Masuala muhimu ya tabia njema yanayo takiwa kuchungwa na kuzingatiwa katika fani mbali mbali za michezo na mazoezi, yanagonga moja kwa moja kwenye maudhui zifuatazao: ubinaadamu, mshikamano na umoja katika mashindano, isafu na uadilifu, khiana, madawa haramu ya kuzalisha nguvu, ustaarabu na tabia za washangiriaji, fungamano lililopo baina ya kocha na wachezaji…[3]

Tabia njema na ustaarabu wenye kuendana na utu, ni kitu chenye tahamani kubwa kabisa kushinda vitu vyote vile katika maisha ya mwanaadamu, kiasi ya kwamba mtu yeyote yule anapokutana na vitendo vya tabia njema, huwa ni mtiifu mwenye kuvipa heshima maalumu vitendo hivyo hata kama yeye mwenyewe atakuwa si mtendaji wa matendo ya tabia njema, ndio maana sisi tukawajibika kusema: “matendo yote yale ya kistaarabu na tabia njema, ambayo ni yenye kuendana sawa na masuala ya michezo, inabidi kuyatumia na kuyafanyia kazi kiwanjani au mazoezini”. Kwa ibara nyengine ni kwamba: mwana michezo anatakiwa asiungalie tu mwili wake nini unahitajia katika uchezaji na mashindano anayo kabiliwa nayo, bali pia anatakiwa kuiangalia roho yake na kuilea katika mazingira mazuri ili kuikamilisha roho hiyo kibinaadamu, kwani kuna uhusiano madhubuti uliopo baina ya roho na kiwiliwili chake. Uislamu haukulitupia macho suala la kuulea mwili tu peke yake, bali umehimiza pia malezi ya kiroho, na ni lazima mwanaadamu awe na vipimo maalumu katika kuulea mwili wake paomoja na roho yake, kwa hiyo kama vile mwili ulivyokuwa na haja ya kulelewa kupitia njia na mfumo maalumu, vile vile roho inahitajia malezi kupitia mfumo maalumu. Baadhi ya njia na mazoezi maalumu yaliyo orodhoshwa katika kuipa roho malezi mema ni: kufunga, kusali, kuomba dua na kadhalika, na kama mtu hakuchukua jitihada za kuulea mwili na roho kwa pamoja, huyo hatukuwa amejilea katika kuuelekea utu na ubinaadamu, hilo basi halitaweza kumtoa yeye katika kundi la wanyama, bali bado atakuwemo humo humo.

 

  Imamu Khomeiny (r.a) pale alipokutana na wanamichezo wa humu nchini, aliwasihi kwa kusema: “wanamicheza wanatakiwa kuyazingatia malezi ya roho zao kama vile wanavyo zingatia suala la kuilea na kuishughulikia miili yao, kwani hilo si jambo jipya. Tokea hapo zamani wanamichezo wa nchi hii walikuwa wakimtaja  Mola wao pamoja na kuukumbuka ushujaa wa Ali (a.s) kwa ajili ya kujihamasisha michezoni mwao, na hilo ndilo lililo watofautisha wao na watu wengine.”[4]

Jambo linalo takiwa kufahamika mbele ya kila mmoja wetu, ni kuwa kila mmoja miongoni mwa wana michezo na vitengo mbali mbali vyenye kushughulikia fani hiyo, wawajibike kisawa sawa katika kuyatambua masuala mbali mbali ya tabia njema na ustaarabu, pia wahakikishe kuwa tabia hizo njema ni zenye kufanyiwa kazi viwanjani, kwani iwapo vitengo vya michezo vitakuwa havina katiba maalumu kuhusu ustaarabu na tabia njema, hilo litamfanya mwana michezo ashindwe kufahamu wadhifa wake kwenye masuala hayo ya tabia njema, au vipi yeye anatakiwa kufungamana na suala hilo.

Ibara zitakazo fuata hapa chini, zina nia na malengo ya kuashiria baadhi ya nyadhifa na tabia njema anazotakiwa mwana michezo kushikamana nazo akiwemo michezoni:

  • Kupambana na nafsi ammara: yaani kupingana na kupambana na matamanio haramu ya nafsi au matamanio ya kishetani, matamanio ambayo huwa ndiyo msingi wa kumuelekeza mja mashakani. Mwana michezo ni kama mwanaadmu mwengine, yeye anatakiwa kupambana na matamanio haramu ya nafsi yake, na hatimae kujiokoa na mashaka yanayo sababisha matamanio hayo haramu.

Kuna Riwaya tofauti zenye kusisitiza suala hili, na miongoni mwake ni kama ifuatavyo:

  1. Mtume Muhammad (s.a.w.w) amesema: “Mwenye nguvu aliye shupavu, si yule mwenye kupambana na mpinzani wake wa mieleka kiwanjani kisha akamtupa chini na kummiliki mpinzani huyo, bali aliye shupavu, ni yule mwenye kuimiliki nasfi yake wakati wa hasira (anapo kasirika)”[5]
  2. Kumenukuliwa habari isemayo kuwa: siku moja Mtume (s.a.w.w) alikuwa akipita sehemu fulani akamuona mtu mmoja mwenye nguvu aliyekuwa akinyanyua jiwe moja zito, na watu wa mtaa ule walikuwa wakimuita mtu huyo kwa umaarufu wa myanyua mawe, likimaanisha jina hilo kuwa yeye ni bingwa wa kunyanyua vitu vizito, pale yeye alipokuwa akinyanyua lile jiwe, watu walikuwa wamesimama na kumuangalia yeye kwa mshangao, Mtume (s.a.w.w) akauliza: mkusanyiko huu ni kwa ajili ya kitu gani? Wale watu waliokusanyika wakaelezea nini kinacho endela, hapo Mtume (s.a.w.w) akasema: hivi nikwambieni ni nani mwenye nguvu zaidi kuliko mtu huyo? Mwenye nguvu zaidi kuliko huyu, ni yule atakaye kasirishwa na kuchokozwa kisha yeye akaweza kustahamili na kuizuiya nafsi yake yenye hamu ya kujibu au kulipiza kisasi kwa lile alilo tendewa, naye akaweza kukaa mbali na shetani wake (nafsi)  pamoja na shetani wa yule aliyemchokoza.[6]
  3. Imamu Ali (a.s) anasema: “Adui mbaya zaidi kwako wewe, ni matamanio ya nafsi yako. Basi jitahidi ili umshinde adui huyo, na ukishindwa! Utaangamia.[7]
  4. Imamu Musa Kaadhim (a.s) amesema: siku moja Mtume (s.a.w.w) aliwambia wale wanajeshi waliorudi kutoka vitani: “Rehema za Mola zitande juu ya wale waliokamilisha jihadi ndogo, na bado jihadi kubwa ni yenye kuwasubiri. Watu wakauliza: hiyo jihadi kubwa ni jihadi gani? Yeye (s.a.w.w) akawajibu: ni jihadi ya kupambana na nafsi.[8]
  • Kuwa na usamehevu: mwana michezo anatakiwa kuwa msamehevu. Pale mwana michezo anapofikia kilele cha ushupavu, wa kuwa na nguvu za kumshinda mpinzani wake, hatakiwi kumtatiza na kumueka mpinzani wake katika mazingira magumu yenye nia ya kulipiza kisasi au kumjeruhi. Yeye anatakiwa kuwa na huruma pamoja na kuwa na moyo wa usamehevu, na amshukuru mpinzani wake kwa ule ushindi alio upata kupitia kwake.

Imamu Ali (a.s) kuhusiana na hilo anasema: “Jitulize ndani ya hasira zako (zizimue hasira zako), na samehe pale unapokuwa uwezo wa kuadhibu, na kuwa na subira pale hasira zinapo kuvaa, na hukumu huku wewe ukijidhatiti kisawa sawa katika nafsi yako, kwani hilo ndilo litakalo kupa wewe hatima njema na kupata malipo kutoka kwa Mola wako”.[9]

  • Kuto kuwa na kiburi: mwana michezo hata kama atakuwa na nguvu kiasi gani, yeye hatakiwi kuwa na kiburi kutokana na nguvu alizokuwa nazo au nafasi maalumu aliyo ipata kutokana na uwezo wake aliokuwa nao. Ni lazima yeye afahamu kuwa: nguvu na uwezo alio kuwa nao unatokana na Mola Muweza.

Pale Imamu Husein (a.s) alipokuwa akipambana na adui zake na kuwashinda alikuwa akisema: “Hakuna nguvu wala aina yoyote ile ya hila (njia) isipokuwa vyote hivyo ni vyenye kutokana na Mweneye Ezi Mungu”[10]

Mola wetu pia katika Qur-ani anatuambia: (Kwa hakika nguvu zote ni za Mola Muweza)[11]

Hakuna sababu basi ya watu wenye nguvu na wana michezo kujifakharisha kutokana na uwezo wa nguvu walizo nazo, bali wao wanatakiwa kuzitumia nguvu hizo kwa ajili ya kutafuta radhi za Mola wao.

Mwisho wa kutakabari ni kuporomoka, mwenye kiburi humdharau mpinzani wake na wala yeye hachukui hatua maalumu za kujihadhari, na natija yake ni kushindwa, kama vile Imamu Ali (a.s) alivyo sema: “Maradhi sugu ya mashujaa mbali mbali, ni kutokuwa na upeo mpana wa kutafakasi”.[12] Na kwa mara nyengine Amesema: “Tatizo sugu kwa wenye nguvu na uwezo, ni kumdharau adui yao”.[13]

  • Kupamba kiheshima na kibinaadamu: moja kati ya mambo muhimu yanayo zingatiwa kwenye michezo, ni kule kupinzana mtu kwa mtu au kundi na kundi (timu na timu), ubinaadamu na tabia njema, ni ngao mbili muhimu zitakazoweza kuudumisha udungu baina ya wana michezo wa timu moja au pia timu zote mbili zinazo pambana, na hili ndilo litakalosaidia kupatikana ukuaji sambamba wa roho na miili ya wana michezo wetu. Kumuangali mpinzani kwa jicho la udugu, ni moja kati ya sifa wanazotakiwa kuwa nazo wachezaji wa  michezo mbali mbali.  Mchezaji hatakiwi kumuangalia mpinzani wake kuwa ni adui wake, kwani hilo litasaidia kupatikana au kujenga uadui baina ya pande mbili za wana michezo hao, jambo ambalo litapelekea kila mmoja kuwa na nia ya kuleta uharibifu na hasara kwa upande wa pili anaokabiliana nao. Mtazamo wa udugu ndio utakao weza kuzitokomeza njama za kishetani kama vile hadaa, uharibifu na khiana kwa wana michezo wa jamii mbali mbali, na hapo ndipo lengo kuu la michezo na mazoezi mbali mbali litakapo kamilika na kuwa imara.

Hivi ndivyo jicho la Uislamu linavyo liangalia suala la mazoezi na michezo katika dira yake. Natumai mtaridhika na jawabu hizi.


[1] Rejea kitabu cha Kipashia, kilichoandikwa na kundi la waandishi kiitwacho, Akhlaqe Kaarbodiy, uk/419, chapa ya Pazjuuheshqaa Ulume Islaamiy, chapa ya pili ya mwaka 1388 Shamsia.

[2] Rejea rejeo iliopita, uk/23.

[3] Rejeo iliopita, uk/80, pia 417, hadi 420.

[4] Sahifeye Imam, juz/18, uk/151.

[5] Biharul-Anwaar, cha Muhammad Baqir Majlisiy, juz/74, uk/153, chapa ya Al-Wafaa, Beirut Lebanon, mwaka 1404 Hijiria. Tuhafu-Uquul, cha Hasan bin Shuu’ba Al-Harraaniy, uk/47, chapa ya Jaamiatul-Mudarrisiin, Qum Iran, mwaka 1404 Hijiria.

[6] Majmuueye-Waraam, juz/2, uk/10.

[7]Ghurarul-Hikami-wa-Durarul-Kalimi, cha Adul-Waahid bin Muhammad Tamiimiy, uk/306, chapa ya Daftari Tabliighaat Islaamiy, Qum Iran, mwaka 1366 Shamsia.

[8] Wasaailush-Shia, cha Sheikh Hurru Al-Aa’miliy, juz/15, uk/161, chapa ya Muassasatu Aalul-Bait, Qum, mwaka 1409 Hijiria.

[9] Nahjul-Balagha, uk/459, chapa ya Daarul-Hijra, Qum Iran.

[10] Al-Luhuufu-a’laa-Qatlit-Tufuufi, cha Sayyid Ibnu Taawuus, uk/119, chapa ya Jihaan, Tehran, mwaka 1348.

[11] Suratul-Baqara, Aya ya 165.

[12] Ghurarul-Hikami-wa-Durarul-Kalimi, uk/259.

[13] Rejea iliyo pita, uk/347.

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI