Please Wait
11148
Mtu atakaeingiliwa na usiku wa Idil-fitri, huku akiwa ni baleghe na mwenye akili timamu, naye akiwa si mtumwa wa mtu wala si fakiri, mtu huyo atawajibika kutoa zakatul-fitri kwa ajili yake na kwa ajili ya wale wote anaowahudumia, na kiwango cha kila mmoja ni kiasi cha kilo tatu za ngano, tende, zabibu, mchele au mahindi au chenye kufanana na vitu hivyo, na zaka hiyo anatakiwa kumpa yule mwenye kustahiki kupewa. Inawezekana pia mtu akaamua kutoa thamani ya kiwango kinachomuwajibikia kutoa.[1] Na wala hakuna tofauti baina ya yule afungae au asiyefunga. Kwa mfano, iwapo mtu aendeshaye nyumba atakuwa si mwenye uwezo wa kufunga, mtu huyo atawajibikiwa kutoa zakatul- fitri kwa ajili yake mwenyewe, pia kuwatolea mkewe pamoja na wanawe pia kuwatolea wale wote walioko juu ya shingo yake.
Rejeo fungamano ni: swali la 6221 (tovuti: 6609) (mahala pa kuzitumia zaka).