advanced Search
KAGUA
13999
Tarehe ya kuingizwa: 2010/07/22
Summary Maswali
hivi ni kwanini baadhi ya watu katika ulimwengu wa ndoto huonekana katika umbile la kinyama, hali ya kuwa wao baadae walionekana kuwa ni miongoni mwa watu waliofaulu na kupata daraja mbali mbali za utukufu.
SWALI
hivi mnaweza kutupa ufafanuzi juu ya visa vya watu mbali mbali vinavyonukuliwa kuhusina na watu hao? Kwani kuna nukuu mbali mbali zinazoelezea kuwa: kuna watu ambao ujanani kwao waliku ni miongoni mwa watu waliojishughulisha na matendo maovu, na baada ya nuru ya Mola wao kuziangaza nyoyo zao, wao walibadilika na kuwa miongoni mwa waumini, kama vile alivyo ongoka Rasuul Turk, ambaye alionekana na mtu mmoja usingizini akiwa na sura ya mbwa aliyesimama kwenye hema la Imamu Husein (a.s) huku akiwa ni mlinzi wa hema hilo aliyekuwa akiwazuia wasiohusika (maadui) kuingia katika hema hilo. Na baada yule mtu aliota ndoto hiyo kumhadithia Rasuul Turki kisa hicho, tendo hilo likawa ndio sababu ya yeye kubadilika na kupata mapinduzi ya kiroho. Pia swali langu linahusiana na kule yeye kuonekana katika ile ndoto huku akiwa na sura ya mbwa, sisi sote tunatambua kuwa: daraja ya mwanaadamu ni kubwa yenye heshima maalumu, kwa nini basi Imamu Husein amkashifu mbele ya wengine katika ule ulimwengu wa ndoto, na kumfanya aonekane akiwa na sura ya mnyama? Kwani hichi ni kisa maarufu kinachotambulikana na kunukuliwa na wanazuoni mbali mbali, name pia ni mtu niliye karibu sana na marafiki waliokuwa na uhusiano na Rasuul Turk, pia mimi mwenyewe nimekisoma kile kitabu kinachohusiana na mtu huyo kiitwacho (Aliyeachwa huru na Imamu Husein (a.s))!!
MUKHTASARI WA JAWABU

Kuna Aya na Riwaya mbali mbali zenye kuonesha kuwa hali na sura halisi za maumbile ya baadhi ya watu ni zenye kutafautiana na lile umbile lao dhahiri wanalo onekana nalo katika ulimwengu huu wa dhahiri. Na mabadiliko hayo huwa yanatokana na yale matendo ya watu hao yalivyo. Miongoni mwa yale matendo yenye kumtoa mtu katika umbile moja kwenda jengine, ni kulewa, ulevi ni moja ya vitu vinavyo weza kumtoa mtu katika umbile lake asili na kumpa umbile la mbwa. Tukiwa katika jitihada za kulijibu swali lako, inapasa kukufahamisha kuwa: si Imamu Husein ndiye aliyemtoa yeye katika umbile lake na kumuonesha mbele ya wengine kwenye ule ulimwengu wa ndoto akiwa katika umbile la mbwa, bali matendo yake ndiyo yaliyo ibadilsha sura na umbile lake la ndani ya nafsi yake. Hivyo basi yeye alionekana katika lile umbile lake ambalo alilivaa kupitia matendo yake maalumu. Pia zingatia kuwa iwapo yeye angelionekana katika picha ya kibinaadamu, basi hilo lingeliweza kumdanganya na kumfanya yeye aamini kuwa ni miongoni mwa watu wema. Lakini vile yeye kuonekana katika umbile la mbwa ndiko kulikomsaidia yeye na kumfanya aathirike na kisa kile na hatimae kutubia.

JAWABU KWA UFAFANUZI

Katika Qur-ani kuna Aya isemayo: (واذا الوحوش حشرت), yaani: (Na pindi wanyama (wakali) watakapo fufuliwa)[1]. Wafasiri wa Qur-ani wameifasiri Aya hii katika maana mbili zifuatazo:

  • Pale wanyama watakapo fufuliwa ili walipizane kisasi pamoja na kutoa ushahidi juu ya matendo ya wanaadamu.
  • Pale wanaadamu mbali mbali watakapo fufuliwa huku wakiwa katika maumbile ya wanyama wakali.[2]

Kwa mara nyengine Qur-ani inatuambia:  (فَلَمَّا عَتَوْا عَنْ ما نُهُوا عَنْهُ قُلْنا لَهُمْ كُونُوا قِرَدَةً خاسِئِين)

Yaani: (Na pale walipokataa kuachana na yale waliokatazwa kuyatenda, hapo tuliwaambia: kuweni katika umbile la makima waliokasirikiwa.)[3] Aya hii inahusiana na wale Waisraili waliokataza kuvua samaki siku ya Ijuumamosi, na pale wao walipokataa kushikama na amri hiyo, Mola aliwageuza makima.

Aya hii inaonesha kuwa: kuna baadhi ya matendo ambayo huwa ni sababu ya kumtoa mtu katika umbile lake halisi na kumueka katika umbile jengine.

Pia kuna Riwaya nyingi kuhusiana na hilo, na sisi tutatoa baadhi ya Riwaya hizo kutoka kwenye baadhi ya vitabu ili kulithibitisha jambo hilo, miongoni mwa Riwaya hizo ni kama ifuatavyo:

  1. Abu Basiir amenukuu kisa kifuatacho kutoka kwa Imamu Baaqir (a.s), pale yeye alipokuwa katika ibada ya Hija pamoja na Imamu Huyo (a.s) akisema:

(Nilimuambia Imamu (a.s): kuna mahujaji wengi walioje mwaka huu, angalia basi jinsi ya sauti zao zilivyo zagaa kila pembe! Imamu (a.s) akajibu kwa kusema: zogo na kelele ni nyingi mno, lakini mahujaji halisi hasa ni wachache walioje. Yeye (a.s) aliendelea kusema: Hivi unahamu zaidi ya kutaka kuufahamu usemi wangu huu kupitia jicho lalo mwenyewe? Baada ya kusema hivyo, Yeye (a.s) aliupitisha mkono wake kwenye macho yangu (aliupangusa uso wangu), kisha akasoma dua fulani, baada ya hapo akaniambia: sasa waangalie mahujaji. Abu Basiir anasema: hapo mimi niliwaona wengi miongoni mwa wale mahujaji wakiwa katika umbile la kima na ngurue, huku wale waumini walio wachache miongoni mwao wakionekana kung’aa kama mfano wa nyota zenye kung’aa  katika usiku wa giza zito.[4]

  1. Riwaya nyengine ni ile isemayo:

(عِدَّةٌ مِنْ أَصْحَابِنَا عَنْ سَهْلِ بْنِ زِيَادٍ عَنِ ابْنِ أَبِي نَجْرَانَ عَنْ مُثَنًّى الْحَنَّاطِ عَنْ كَامِلٍ التَّمَّارِ قَالَ سَمِعْتُ أَبَا جَعْفَرٍ ع يَقُولُ النَّاسُ كُلُّهُمْ بَهَائِمُ ثَلَاثاً إِلَّا قَلِيلًا مِنَ الْمُؤْمِنِينَ وَ الْمُؤْمِنُ غَرِيبٌ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ)

Maana yake kwa ufupi ni kwamba: Imamu Baaqir (a.s) amesema: (Wengi miongoni mwa wanaadamu ni wanyama,  isipokuwa wachache tu miongoni mwao ndio waumini, na tambueni kuwa: muumini ni mgeni (ni mtu anayetengwa), Yeye (a.s) aliyakariri maneno hayo mara tatu.)[5]

 

Riwaya hii inatufafanulia wazi kuwa: wengi miongoni wa watu wanao onekana kidhahiri kuwa ni wenye maumbile ya kibinaadamu, si wanaadamu halisi, bali maumbile na sura zao halisi ni zile sura na maumbile ya kinyama ziendayo sawa na amali zao.

  1. Na miongoni mwa Riwaya nyengine, ni ile iliyo pokewa kutoka kwa Mtume mwenyewe (s.a.w.w), isemayo: (Ndani ya umma wangu kutatokea maporomoko na malembeo, (yaani watu wataporomokewa na kufinikwa na ardhi, kama vile leo watu wanavyo angushiwa juu yao mabomu na silaha nzito nzito), Masahaba wakamuuliza: ni wakati gani yatakapotokea matokeo hayo? Yeye (s.a.w.w) akawajibu: hayo yatatokea pale watu watakapojishughulisha na upuuzi wa kuwakusanya wanawake katika vikao vya muziki pamoja wao kujishughulisha na kulewa na kustarehe kinyume na maadili mema. Basi naapa kwa Mola kuwa: watu hao wa umma wangu watajishughulisha usiku na mchana na upuuzi na uasi, huku wakiwa tayari Mola wao ameshawabadilisha na kuwaweka katika maumbile ya kima na nguruwe, na hilo linatokana na kule wao kuyageuza yale ya halali kuwa ni haramu, na ya haramu kuwa ndiyo ya halali, huku wao wakilewa katika vikao walivyo waalika ndani yake wanawake kuja kuwaimbia, pia msiba huo utawakuta kwa kutokana na wao kula riba na kuvaa nguo za hariri.[6]

Pia Riwaya hii ni yenye kututhibitishia kuwa: kuna matendo ambayo yanasababisha maumbile ya ndani ya mwanaadamu kubadilika.

Mpaka hapa sisi tumeweza kupata ithibati kuhusiana na suala hili, na ithibati hizo zimechukuliwa moja kwa moja kutoka katika Aya na Riwaya maalumu zilizoweza kututhibitishia kuwa: maumbile ya ndani au ya nje ya baadhi ya watu hubadilika kutoka katika maumbile ya kibinaadamu na kuenda katika maumbile ya kinyama, na hilo huwa linasababishwa na amali zao wenyewe.

Jawabu ya swali la mwanzo tayari tumeshaipata ufumbuzi, na kilichobakia hapa, ni kuelekea katika swali lako la pili lililosema kuwa: ni kwa nini Rasuuli Turk alionekana katika ulimwengu wa ndoto akiwa na umbile la kinyama?

Jawabu ya suala hili ni kwamba: yeye alikuwa ni mnywaji pombe aliyekomaa katika amali hiyo, kwake yeye kunywa pombe ilikuwa ndio ada yake, naye alifurutu ada katika amali hiyo, pia yeye alkuwa haachani na amali hiyo isipokuwa ndani ya mwezi wa Muharram tu, hii ni kwa sababu ya yeye kumheshimu sana Imamu Husein (a.s). Ni vyema pia wewe ufahamu kuwa kudumu katika pombe, ni moja kati ya yale maovu yenye kuibadilisha sura halisi ya ndani ya nafsi ya mwanaadamu, na iwapo sisi tutalifahamu hilo, itabidi kufahamu kuwa matendo yake mwenyewe ndiyo yaliyosababisha yeye kuonekana katika ile sura na umbile la kinyama.

Kwa hiyo Imamu Husein (a.s) siye ileibadilisha sura na umbile la Rasuul Turk, bali yeye mwenyewe ndiye aliye itengeneza sura na picha yake ya ndani na kuifanya iwe katika umbile la kinyama.

  Ama kuhusiana na kile kipengele cha swali lako lililosema kuwa: ni kwa nini Imamu Husein (a.s) hakumstiri mtu huyu, hali ya kuwa mwanaadamu kidhati na kiasili, ni kiumbe aliye na daraja kuu, hapa yabidi sisi kukujibu kupitia vipengele vifuatavyo:

  • Tendo hilo la Imamu Husein (a.s) lilitaka kumfahamisha yeye kuwa: ingawaje yeye ni muovo, lakini bado kwa kutokana na yeye kumuekea Imamu Husein (a.s) aina maalumu ya staha, na kule yeye kuhudhuria katika maombolezo ya Imamu huyu (a.s), basi yeye pia anastahiki kukirimiwa, na hilo ni lenye kuonesha ukarimu wa Imamu Husein (a.s) ulivyokuwa ni mkubwa, pia hilo ni funzo kwa wanaadamu kuto wafukuza na kutowaona uchafu wale wanaotenda maovu, bali ni kuwakaribisha na kuwaweka karibu, kwani wao huenda wakaongoka kupitia tabia na ustaarabu wa watu wema.
  • Jengine ni kwamba: iwapo yeye asinge iona hali halisi aliyokuwa nayo kutokana na matendo yake, basi angeliweza kujidanganya kuwa yeye ni mtu mwema asiye na tatizo.
  • Imamu (a.s) alikuwa akiitambua vilivyo nafsi ya Rasuul Turk ilivyo, hivyo Imamu Husein (a.s) alitaka kumuelekeza mja huyu kwenye ile njia ambayo alitakiwa kuifuata, Naye (a.s) alifanya hivyo kwa kule kuuona muelekeo wa mja huyu alio kuwa nao ndani ya nafsi yake. Na hilo linaonesha kuwa nafsi ya mtu huyu ilikuwa ina aina fulani ya muelekeo, na ilikuwa ikisubiri tu kupata aina fulani ya msukumo ili ielekee kwenye mlolongo wa watu wema. Na wala hakuna lawama zozote zenye kumuelekea yeye baada ya yeye kutubia kisawa sawa mbele ya Mola wake, nasi hilo tumelisoma kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) pale aliposema:

 (التائب من الذنب کمن لا ذنب له), yaani: (mwenye kutubia kutokana na dhambi zake, mfano wake ni mfano wa yule aliyekuwa hakufanya dhambi kabisa.)[7]

Pia katika swali lako kunaonekana kuwepo wasi wasi juu ya kuwa: ni vipi Imamu Husein (a.s) alimkubali mtu huyu hali ya kuwa yeye ni mwenye sura na umbile la mbwa?

 Jawabu ni kwamba: ni kweli Rasuul Turk alikuwa na sura ya mbwa, lakini yeye alikuwa ni mbwa aliyekuwa akifanya jitihada za kulilinda hema la Imamu Husein (a.s), vipi basi Imamu (a.s) amfukuze au asimjali! Hebu wewe iangalie nafsi ya Imamu Husein (a.s) na ukarimu wake! Ni kweli alikuwa na sura ya mbwa, lakini yeye alikuwa ni mbwa mwenye heshima aliye uwekae heshima mwezi wa Muharram kwa kutokana na tokeo lilitokea ndani ya mwezi huo, naye alikuwa akiwakataza wenziwe pamoja na watu wengine na kuwataka waachane na amali ya kunywa pombe na kufanya uasi ndani ya mwezi wa Muharram, na ile sura ya mbwa ilikuwa ni sifa mbaya iliyohitajia kuondolewa, na baada ya yeye kutubia, sura yake ya ndani ilibadilika na kuelekea katika nuru ya Mola wake. Hiyo ndiyo hali halisi ya hatima ya mtu huyu ilivyokwenda.

Tunamuomba Mola atuwafikishe katika kheri na matendo mema.


[1] Aya ya 4 ya Suratut-Takwiir.

[2] Al-Fawaatihul-Ilaahiyya-wal-mafaatihul-ghaibiyya, cha Nii’matu-LLahi bin Muhammad, juz/2, uk/487, chapa ya Daru Rikaabiy, Cairo, mwaka 1999 Miladia.

[3] Suratul-Aa’raaf, Aya ya 166.

[4] Biharul-anwaar, juz/27, uk/30, chapa ya taasisi ya uchapishaji ya Al-Wafaa, Beirut Lebanon, mwaka 1404.

[5] Al-Kafi, juz/2, uk/242, mlango kuhusu uchache wa waumini.

[6] Tarjama ya juzu ya 5 ya kitabu Biharul-anwaar, uk/248, mlango wa 24  wenye kuhusiana na mawaidha maalumu ya Imamu Sadiq (a.s), chapa ya taasisi ya uchapishaji ya Islaamiyya.

[7] Wasailush-Shia, ju/16, uk/75, chapa ya taasisi ya uchapishaji ya Aalul-Bait, mwaka 1409.

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI