advanced Search
KAGUA
15869
Tarehe ya kuingizwa: 2006/06/03
Summary Maswali
Nini maana ya Feminism?
SWALI
Nini maana ya Feminism?
MUKHTASARI WA JAWABU

Neno (Feminism) linatokana na lugha ya Kifaransa ambalo asili yake ya Kilatini ni (Femind), neno hili hutumika katika lugha mbali mbali huku likiwa na maana moja inayomaanisha uke au jinsia ya kike, ijapokuwa neno hili linapotumika kutoka lugha moja kwenda nyengine huonekana kuwa na mabadiliko kidogo ya kimaandishi lakini bado huwa limebeba maana ile ile ya uke.

Neno (Feminine) huwa lina maana ya uke au kitu chenye sifa ya uke, na neno (Feminism) laweza likawa na aina mbili za maana, ya kwanza ni ile yenye kumaanisha fikra maalumu za utetezi wa haki sawa baina ya wanawake na wanaume katika nyanja tofauti za kijamii, kiuchumi na kisiasa.

 

Baada ya kupita kipindi si kirefu cha kuzuka au kuanzishwa fikra za Kifeminism, kuliweza kupatikana vyama na makundi mbali mbali yenye kudai utetezi wa haki za wanawake, huku kila mmoja akiwa na malengo maaalumu katika madai yake. Maana ya pili ya neno hili huwa inamaanisha upatikanaji wa sifa za kike ndani ya jamii ya kiume, sifa ambazo humfanya mwanamme kufanana na mwanamke kitabia, nasi katika maandiko haya hatutogusia maana hii ya neno hili, bali lengo hasa ni kuizungumzia maana ya kwanza ya neno hili.

 

Chimbuko la utumikaji wa neno (Feminism) likiwa neno hili ni lenye kumaanisha fikra maalumu za haki sawa kwa wake na waume, linarudi si chini ya miaka mia mbili iliyopita, lakini twaweza kusema kuwa chimbuko hasa la fikra hizi limeanza ndani ya Karne ya kumi na tisa miladia. Fikra za Kifeminism zilitawanyika na kujijenga katika sura mbali mbali kwa ajili ya kuhakikisha kuwa, malengo ya fikra hizi ni yenye kukubalika ndani ya jamii mbali mbali. Ukamilikaji na upeaji wa fikra hizi ulikamilika katika hatua mbili, hatua ya kwanza ni kuanzia Karne ya 19 hadi mwaka 1920 (baada ya vita vya kwanza vya dunia), na hatua ya pili ya ukamilikaji wake ilikuwa ni ndani ya miaka ya sitini na kuendea mbele. Mara ya kwanza kabisa ya neno (Feminism) kupata maana maalumu inayomaanisha utetezi wa haki za wanawake ilianzia America. Fikra hizi zilianzishwa ili kukabiliana na ubaguzi uliopatikana ndani zama hizo uliokuwa ukimbaguwa mwanamke katika haki tofauti kwa kutokana na hali yake ya kijinsia aliokuwa nayo, katika hali kama hiyo ndipo baadhi ya wanaharakati wenye fikra maalumu za kijamii au kidini walipoamua kukabiliana na gurudumu hilo la ubaguzi na unyanyapaa wa wanawake.

Haidhuru harakati hizo hazikuacha kuwa na aina fulani ya udhaifu, lakini katika mika ya 1970 hadi 1980 harakati za fikra hizo ziliweza kujengeka katika makundi mbali mbali ya Kifeminism, pia kulionekana kupatikana makundi mengine ya kisiasa yalioweza kuathiriwa na fikra hizo, makundi ambayo hayakutarajiwa kujiunga na fira hizo hapo mwanzo, hii ni kwa kutokana na makundi hayo kushikamana na fikra za kuto kubali ani yeyote ile ya mageuzi ya kisiasa huko Uingereza mnamo Karne ya 18 hadi 19, na hatimae fikra hizo ziliweza kuvuka mipaka na mwishowe zikaweza kuingia ndani ya fikra za kidini na kimadhehebu.

La muhimu kuligusia hapa ni kwamba, makundi ya Kifeminism ni yenye kutofautiana katika baadhi ya mitazamo yake, huku wote wakiwa ni wenye kukubaliana kuwa “haki za wanawake ni zenye kukiukwa ndani ya jamii, kwa hiyo ni lazima kutumike njia maalumu katika kukabiliana na hali hiyo”. Haidhuru wao ni wenye kukubaliana katika hilo lakini bado huwa ni wenye kutofautiana kimitazamo, jambo ambalo huwa linawafanya wao kugawika katika makundi tofauti.

Feminism imegawika katika makundi tofauti, na miongoni mwa makundi hayo ni:Liberal fenimism, marxist feminism, Social feminism, Radical feminism na Islamic feminism.

Feminism iliyoweza kusambaa na kuchukua nafasi maalumu ndani ya jamii za kiisalmu ni Feminism ya kijamii, Feminism ambayo kitarehe ni yenye mizizi iliopea zaidi, ambayo fikra zake zilianza kuenea ndani ya jamii mbali mbali za kiislam mwishoni mwa Karne ya 19. Fikra za Kifeminism ziliweza kuchukua nafasi maalumu ndani ya jamii za kiislam kwa kupitia jina la (Women’s studied) yaani utafiti kuhusiana na hali halisi ya wanawake, nalo hilo lilikuwa ni somo maalumu lililoweza kupenya ndani ya mfumo wa kielimu unaofuatwa na nchi mbali mbali za kiislamu, mpango ambao ulioletwa na wafuasi wa fikra za Kifeminism, na hatimae mpango huo ukawezaliweza kuzalisha watafiti wa masuala mbali mbali yanayohusiana na wanawake.

 

Linalotakiwa kuzingatiwa hapa ni kwamba, kuzaliwa kwa fikra za Kifeminism ndani ya jamii za Kimagharibi kulitokana na hali maalumu ya kijamii iliyokuwepo ndani ya zama za uzukaji wa kila moja kati ya makundi ya Kifeminism, la busra basi ni kufanya uchunguzi juu ya sababu za kuzaliwa kwa makundi hayo, ili kuweza kukabiliana nayo kijawabu katika majadiliano kuhusu madai na fikra za makundi hayo zinazoelekezwa na kusambazwa ndani jamii zetu.

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI