Please Wait
11096
Jawabu kutoka ofisi ya Ayatullahil-Udhmaa Sistani (Mola amlinde):
1-mwanamke ambaye ananyonyesha, aliye na uchache wa maziwa, awe ni mama wa mtoto au mlezi anayelipwa kwa ajili ya kumnyonyesha mtoto huyo, au hata kama atakuwa anamnyonyesha bure, iwapo funga itakuwa ni yenye kumletea madhara au kumletea mtoto madhara, yeye hatowajibika kufunga, na badala yake atatakiwa kila siku moja kumpa fakiri kiasi cha gramu 750 za chakula, pia tatakiwa kuzilipa funga hizo baadae, lakini ni wajibu kuchukuwa hadhari na kutumia hukumu hii pale tu iwapo kutakuwa hakuna njia nyengine ya kutumia kwa ajili ya kumnyonyesha mtoto huyo, lakini iwapo kutaweza kutumika njia nyengine, kama vile kumtafuta mtu wa kuweza kupokezana naye katika kazi hizo ya unyonyeshaji, hapo kutakuwa na mushkeli kuitumia hukumu hii. Na iwapo yeye atachelewa kuzilipa funga zake hadi mwaka mwengine, basi atatakiwa kuzilipa pamoja na kuzitolea fidia mara mbili ya kiwango cha gramu 750 za chakula kwa kila siku moja, fidia ya kwanza ni ya kula na fidia ya pili ni ya kuzichelewesha. Na iwapo yeye atazidi kuchelewesha zaidi katika ulipaji wa funga hizo, basi hakuna adabu ya kuengezeka fidia juu yake. Naona jawabu iko wazi kabisa.
Ofisi ya Ayatullhil-Udhmaa Makarim Shiraziy (Mungu amhifadhi):
Mama yeyote yule ambaye atahukumiwa kuwa: funga ni yenye kumletea madhara yeye au mtoto, au itamsababishia kukauka maziwa yake, awe mama wenyewe ni mama mzazi au mlezi tu, yeye hatokuwa na wajibu wa kufunga, lakini anatatakiwa kutoa fidia ya gramu 750 ya chakula na kumpa fakiri kwa kila siku ambayo ameacha kufunga, na pia atatakiwa kuja kuzilipa funga hizo baadae.
Ofisi ya Ayatullhil-Udhmaa Safi Gulpeiganiy (Mungu amhifadhi):
1- mama huyo atatakiwa kutoa gramu 750 za chakula na kumpa fakiri kwa kila siku ambayo hakufunga, na pia atatakiwa kutoa tena kiwango kama hicho cha fidia kwa mara nyengine kwa ajili ya kuto weza kuzilipa funga hizo kwa wakati, kwa kule kuendelea kunyonyesha kwa mwaka wa pili mfululizo.
2- kama makusudio ya swali lako ni kwamba je yeye akizidi kuzichelewesha na kuto zilipa funga hizo, hivi fidia yake itazizi mara mbili? Jawabu: ni hapana bali atatakiwa kuzilipia fidia mara moja tu.