advanced Search
KAGUA
7517
Tarehe ya kuingizwa: 2009/11/26
Summary Maswali
nini ilikuwa hatima ya farasi wa Imamu Husein (a.s) huko Karbala?
SWALI
katika vita vya Karbala nini ilikuwa hatima ya farasi wa Imamu Husein (a.s) aliyejulikana kwa jina la Dhul-Janaah?
MUKHTASARI WA JAWABU

Waandishi mbali mbali wa walioandika na kulizungumzia tokeo la Karbala, hawakutoa ufafanuzi wa kutosha kuhusiana na farasi wa Imamu Husein (a.s), bali walichokielezea ni kuwa, farasi  huyu alijipakaa damu ya Imamu Husein (a.s), kisha akaelekea kwenye mahema huku akitoa sauti kali yenye kuashiria huzuni na hasira. Watu wa nyumbani kwake ambao wakuwa wamo kwenye mahema, walipoisikia sauti ya yule farasi, walitoka nje ya mahema hayo, na walipomuona yule farasi yuko katika hali ile, walifahamu kuwa Imamu  Husein (a.s) tayari ameshauwawa.[1] Lakini baadhi ya waandishi wa hivi sasa wameelezea khabari nyengine kuhusiana na hilo, na miongoni mwa vitabu vilivyo elezea khabari za nyongeza kuhusiana na hilo, ni (Naasikhut-Tawaariikh) kilichoelezea kuwa, farasi huyu alisimama nje ya mlango wa kungia katika mahema, kisha akawa anakitwanga kichwa chake na ardhi hadi akafariki, na baadhi ya waandishi wengine wamesema kuwa, farasi huyu baada ya kuuwawa kwa Imamu Husein (a.s), alielekea katika mto Furaat kisha akijtupa ndani ya  mto huo.[2]

 


[1] Rejea kitabu Aamaal cha Sheikh Saduuq, uk/163.

[2] Rejea kitabu Naasikhut-Tawaariikh cha Mirza Muhammad Taqiy Sepehriy, juz/6, uk/2.

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI