Please Wait
7454
Suala hilo limenukuliwa kutoka sehemu tofauti:
1- Imenukuliwa katika maneno ya Zainab (a.s) yaliyosema: “Ewe Muhmmad (s.a.w.w), wanao wa kike wamefanywa kuwa ni mateka, na wanao wa kiume wameuwawa, na upepo unavuma juu ya miili yao, na huyo hapo Husein (a.s) yupo chini hali akiwa amekatwa kichwa kwa kisogoni…”[1]
2- Kutoka kwa Imamu Sajjaad (a.s) yamenukuliwa maeno yafuatayo: “Mimi ni mwana wa yule aliyekatwa kichwa kwa kisogoni…”[2]
3- Kuna maandiko yenye kunukuu aina za salamu anazozisoma Imamu Mahdi (a.s) pale anapomsalia na kumsalimia Imamu Husein (a.s), yasemayo: “Sala na salamu ziwe juu ya yule aliyechinjwa kupitia kisogoni kwake…”[3]
[1] Bihaaru-Anwaar cha Muhammad Baaqir Majlisiy, juz/45, uk/59, chapa yenye mijalada 110 ya Daarul-Wafaa, Beirut Lebanon, mwaka 1404 Hijiria, pia rejea kitabu (Al-luhuuf) cha Ibnu Taawuus, uk131, chapa ya Jihan Tehran, mwaka 1348 Shamsia, pia rejea kitabu (Al-Manaaqib) cha Ibnu Shahr Aashuub Mazandaraniy, juz/4, uk/113, chapa ya Allaama yenye mijalada minne, Qum Iran, mwaka 1379 Hijiria.
[2] Bihaarul-Anwaar, juz/45/ uk/175.
[3] Bihaarul-Anwaar, juz/98/ uk/318, Hadithi ya 8.