Please Wait
9358
Kitabu (Dam-us-sajuum) ni tarjama ya kitabu maarufu cha maombolezo kinachotokana na Haaj Sheikh Abbaas Qummiyi, ambaye ni muandishi wa kitabu Mafaatihul-jinaan. Kitabu (Dam-us-sajuum) kimepigwa chapa na kitengo cha uchapishaji cha Hijrat kilichoko Qum Iran mwaka 1386 Shamsia, chini ya jina la (Dam-us-sujuum-fii-maqtal-Sayyidunal-Husein Madhluum (a.s)). Kitabu (Nafsul-humuum) asili yake kimeandikwa kwa lugha ya Kiarabu, na Allaama Shaa’raniy (r.a), ndiye aliyefanya kazi ya kukitarjumu kitabu hicho kutoka kwenye lugha ya Kiarabu kwenda Kifarsi, huku yeye akionekana kutoa baadhi ya ufafanuzi kwenye baadhi ya vipengele na ibara alizozifasiri au kuzitarjumu kutoka katika lugha mama ya kitabu hicho, na miongoni mwa zile ibara zilitolewa ufafanuzi na mfasiri huyu, ni hili shairi ambalo muulizaji wetu amelielekea na kuuliulizia uhakika wake na wapi yeye anaweza kupata nukuu za shairi hilo, na baadhi ya maana ya shairi hilo ni kama ifuatavyo:
Mfalme wa wote ametupwa chini, hadi taji lenye kupendeza (kichwa cha Mimamu Husein (a.s) likaonekana kung’aa juu ya kichwa cha mshale, mara nuru ya medali yenye thamani itokanayo na taji hilo ikaupamba mshale huo kwa nuru isio na kifani…, kichwa kile hakikuwa ni kichwa tu kwenye jicho la yakini, bali ni shina na kibla kinachoelekewa na nyoyo zenye kufuata taa ya upendo.
Huu basi ndiyo ufafanuzi juu ya swali lako, tunataraji jawabu yetu itakuwa ni yenye kuwatosheleza wasomaji wetu kuhusiana na swali lililoulizwa hapo juu.